WATAFUTIENI MASOKO VIJANA WANAOPATA ELIMU NJE YA MFUMO USIO RASMI- KHALID

Angela Msimbira SONGWE

Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeshauriwa kuhakikisha vijana wanaopata elimu nje ya mfumo usio rasmi wana tafutiwa masoko ili kupunguza wimbi la vijana wanaozurura mitaani kwa kukosa muelekeo wa maisha.

Rai hiyo imetolewa leo Oktoba 29, 2024 mkoani Songwe na Naibu Katibu Mkuu Utawala, Wizara ya Elimu na Mafunxo ya Amali Zanzibar, Khalid Masoud Waziri wakati kufunga kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za programu ya kuhudumia watoto  UNICEF katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Songwe.

Amesema kuwa Serikali imeamua kuanzisha mpango wa elimu changamani kwa vijana walioko nje ya shule IPOSA kwa lengo la kutoa ujuzi, lakini ipo haja ya viongozi wa mikoa na halmashauri kuhakikisha wanawatafutia masoko ya bidhaa wanazozitengeneza ili ziwaongezee kipato na kujiatia ajira.

‘Vijana wa IPOSA wakipata ujuzi na kuwaacha bila kuwatafutia ajira wanarudi mitaani, hivyo ni wajihu wa kila kiongozi ngazi ya mkoa na halmashauri kujiuliza baada ya vijana hao kupata ujuzi nini kifanyike ili vijana hao wawe na manufaa kwa taifa.”
Khalid pia amezitaka halmashauri kuhakikisha wanabuni viwanda vidogo vidogo ambavo vitawasaidia vijana hao kupata ujuzi utakaowawezesha kujikwamua kimaisha na kuacha kuzurura mitaani bila kazi.

Aidha, amezitaka IPOSA na ZIPOSA kukaa chini kwa pamoja na kuja na mpango mkakati wa mashirikiano ya pamoja katika kuhakikisha wanakuwa na masoko kwa vijana hao waliopo nje ya mfumo rasmi wa shule kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Elimu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Susan Nussu amesema kuwa lengo la kikao kazi hicho ni kuwajengea uwezo maafisa elimu wa mikoa na halmashauri kuhusu utekelezaji wa  miradi ya UNICEF pamoja uwekaji wa mpango wa bajeti wa mwaka 2025/2026.

Vilevile mwakilishi kutoka wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Frank Angusi amesema Serikali itaendelea  kuweka mazingira wezeshi ili wadau mbalimbali wa elimu kushirikiana kwa pamoja  katika kutekeza mfumo mzima wa elimu nchini.

Related Posts