MERIDIANBET IMERUDISHA KWENYE JAMII TENA

KAMPUNI ya Meridianbet imefanikiwa kurudisha kwenye jamii kwa mara nyingine leo pale ambapo ilifika Kijitonyama Ali Maua jijini Dar-es-salaam na kufanikiwa kutoa msaada kwa familia ambazo zina uhitaji katika eneo hilo.
Meridianbet wameendelea kua mstari wa mbele kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii yao haswa katika wale watu wenye uhitaji, Leo wamefanikiwa kutoa msaada kwa familia mbalimbali ambazo zinapitia wakati mgumu katika eneo la Kijitonyama Ali Maua.
Kampuni hiyo kongwe imefanikiwa kutoa mahitaji ya nyumbani kwa familia hizo zinazopitia changamoto na mahitaji ambayo wametoa ni kama Sukari, Mafuta, Mchele, Unga wa Ngano, pamoja Sabuni.
Meridianbet wameendelea kua mfano wa kuigwa kwa kuendelea kuhakikisha jamii yake inanufaika na uwepo wao, Kwani huu ni utaratibu ambao wamekua nao miaka na miaka sasa kuhakikisha jamii yake inanufaika na kile ambacho wamekua wakivuna.
Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa katikati ya wikii hii ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko ndani ya Meridianbet Bi Nancy Ingram alipata nafasi ya kuzungumza machache katika hafla hiyo “Tunafuraha leo sisi kama Meridianbet kuleta furaha na tabasamu katika hizi familia, tunatambua umuhimu wa kuwa na mahitaji ya nyumbani, maana bila mahitaji haya familia haiwezi kuishi wala kufanya kazi, tumeweza kuwashika kidogo mkono familia na zoezi hili ni endelevu kuwashika mkono familia zenye changamoto kama hizi”
Aidha wakazi wa eneo la Kijitonyama eneo la Ali Maua ambao wameweza kupata msaada huo kutoka Meridianbet wameweza kuzungumza machache lakini kubwa zaidi ni kutoa shukrani kwa kile walichopokea, Huku wakitoa wito kwa makampuni mengine kuiga kile ambacho kinafanywa na mabingwa hao wa michezo ya kubashiri.

Related Posts