Nchi 128 kuishuhudia Tanzania pokea mastaa wakubwa Afrika na kuzigawa tuzo 2025

Msimu wa Pili wa Tuzo za Trace Music Awards & Summit umezinduliwa Rasmi leo na Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Tanzania, Zanzibar huku Muziki wa Bongofleva ukipewa heshima kubwa kwa kuweka kipengele maalumu Katika Tuzo hizo na kuwapa nafasi wasanii wa Bongofleva kupata mashavu na kutangaza Muziki wao international

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika February 24-26 mwaka 2025 na sitafanyika visiwani Zanzibar huku likitarajiwa kuwa tamasha la aina yake litakaloshuhudiwa nchi zaidi ya 120 kupitia channel ya Trace ambao Ndio waandaji wa Tuzo hizo huku tamaduni za watanzania zikitawala kutokana na kufanyika kwa tamasha hilo Zanzibar

Kama utakumbuka Trace Awards msimu uliopita ilifanyika Rwanda na ikashuhudiwa Burudani kubwa na wasanii wakubwa kama Davido, Diamond, Rema, Jux na wengine walioperform na kunogesha tamasha hilo.

Related Posts