Rais Samia ashiriki mjadala kuhusu Kilimo barani Afrika uliofanyika, Des Moines, Iowa nchini Marekani

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki
kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika, katika
Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 30 Oktoba, 2024. Mjadala
huo ambao uliandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ulihudhuriwa na
viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani
hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza
kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo Barani Afrika pamoja
na Nishati Safi ya Kupikia katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini
Marekani tarehe 30 Oktoba, 2024. Kushoto ni Rais wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akimsikiliza. Rais Dkt. Samia alishiriki
mjadala huo kando ya mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung ambao
umeandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation

Viongozi
mbalimbali wakifuatilia mjadala kuhusu Kilimo Barani Afrika katika Mji wa Des
Moines, Iowa nchini Marekani kando ya mjadala wa Kimataifa wa Norman E.
Borlaung ambao umeandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation tarehe 30
Oktoba, 2024.

 

 

Related Posts