Trump apiga kampeni kwenye gari la taka taka

Donald Trump ameonekana akitumia njia za kipekee na zenye utata katika kampeni zake baada ya kuonekana kwenye Gari la Taka akiwa na ujumbe kwa Wapinzani wake wa Chama cha Democratic, Rais Joe Biden pamoja na Makamu wake Kamala Harris, Trump alishuka kwa mbwembwe kutoka kwenye Ndege yake binafsi akiwa na vesti ya usalama yenye rangi ya machungwa na njano, kisha akaingia kwenye kiti cha abiria kwenye Gari hilo la Taka ambalo limeandikwa jina lake.

Kwa mujibu wa Wachambuzi wa siasa Nchini Humo wameeleza kuwa hatua hiyo ni majibu kwa kauli ya hivi karibuni ya Rais Biden aliyosema, “taka pekee ninayoiona ni wafuasi wa Trump” hivyo kwa kujibu, Trump alionekana akisema “Gari hili ni kwa heshima ya Kamala na Joe Biden,” akionesha dhihaka mbele ya wafuasi wake

Kitendo hicho cha Trump kimezua hisia za Watu mitandaoni, ambapo baadhi ya watu wakiunga mkono mbinu yake ya kisiasa ya kujiweka karibu na watu wa kawaida, huku wengine wakimkosoa kwa kuchochea mgawanyiko, Trump aliendelea na kampeni zake kwa kusisitiza kwamba “hakuna mtu anayeweza kuwadharau wafuasi wake” na kuongeza kuwa, anawaunga mkono Raia wote wa Marekani kwa nguvu zake zote.

 

Related Posts