Tanzania Yasheherekea Siku ya Shampeni kupitia Kinywaji maarufu cha Moët & Chandon

MOËT & CHANDON wameadhimisha Siku ya Shampeni kwa hafla ya kusisimua iliyofanyika kwenye ghorofa ya juu kabisa ya Hoteli ya Kifahari ya Hyatt Regency. Hafla hiyo ililenga kusherehekea “Ubunifu usio na mwisho katika ufundi,” ukiwaleta pamoja wabunifu, waundaji, na watengeneza mitindo ya mavazi, wakiwemo Juma Jux, Ommy Dimpoz, Mtani Bespoke, Kiki Fashion, Branoh Bahati, Victoria Martin, George Williams, Seko Shamte, Grace(Nyumba ya kifahari ya mtindo. ),Howard,Bianca Mengsen,Pedaah John, Arjun, Mgece na Rio Paul.

Mtani Bespoke, mbunifu na fundi cherehani mashuhuri, alitumia hafla hiyo kuelezea safari yake aliyoifanya Épernay, Ufaransa, katika wasilisho maalum la video iliyonasa matukio muhimu aliyoyafanya yeye na mafundi wengine wa Kiafrika waliokutana kujifunza na kufahamu ubora wa Moët & Chandon kuanzia kutengenezwa kwake hadi kuingia sokoni. Kwa kutilia mkazo safari hii, Mtani alitengeneza na kuzindua suti maalum ambayo ilinakshiwa kwa ustadi na urithi wa Tanzania na urithi wa Moët & Chandon, ikijumuisha uwepo wa mashamba ya zabibu kama yale yanayotengeneza shampeni ya Moet and Chandon pamoja na utamaduni wa Kitanzania kupitia urithi wa mavazi ya jamii ya Wamasai. “Kupitia kipande hiki, nilitaka kuheshimu makuzi yangu na msukumo niliopata nilipofika Épernay. Ni muunganiko wa walimwengu wawili ambao, kwa pamoja, wanasherehekea ufundi wa kweli,” Mtani alisema.

Janet Mwalilino ambaye ni Mwakilishi wa Chapa ya Moet na Hennesy alifungua jioni hiyo, akisema, “Kaulimbiu ya usiku wa leo, ‘Ubunifu Usio na Mwisho katika Ufundi,’ inaonyesha ari yetu ya kuinua nyakati za maisha kwa shampeni na kutumia usanii wetu wa kipekee tulionao. Urithi wa Moët & Chandon umejengwa katika kuchanganya mila na uvumbuzi, na tunafurahi kushiriki hili na jumuiya yetu ya Kitanzania.

Mshehereshaji Rio Paul aliongoza hafla ya jioni, akihakikisha anatumia uzoefu wake muda wote ili kufanya watu waburudike. “Inatia moyo kuona utamaduni wetu wa Kitanzania ukiheshimiwa kupitia ushirikiano na kinywaji hichi maarufu. Usiku wa leo, tunasherehekea talanta na hadithi za kipekee za watu wote tuliopohapa, “alisema.

Jioni ilihitimishwa kwa onyesho la kupendeza na kuvutia la violin na Agustino, huku wageni wakifurahia kwa pamoja na kubadilishana mawazo kuashiria matukio yao muhimu ya pamoja. Tukio hili la kukumbukwa lilisisitiza dhamira ya Moët & Chandon katika sanaa, ubunifu kwa kushirikiana na watu wa nchini Tanzania, kuunganisha ushawishi wa Kiafrika na Kifaransa.

Related Posts