KOCHA wa zamani wa Yanga na Azam FC, Hans Pluijm amekifuatilia kikosi cha Simba na kushangazwa na namna straika mpya wa timu hiyo, Steven Mukwala alivyoanza na kasi ndogo, kisha kumpa akili mpya akisisitiza anaimani akikaa vizuri Msimbazi watashangilia mabao ya kutosha kutoka kwake.
Mukwala amefikisha mabao mawili baada ya jana Jumamosi kufunga dhidi ya Mashujaa.
Pluijm aliyeandika rekodi kadhaa tamu akiwa na Yanga, ameliambia Mwanaspoti kwamba ana imani kubwa na Mukwala akisema licha ya changamoto zinazomkabili mwanzoni, lakini ana uwezo wa kui-saidia Simba.
Pluijm anayemfahamu Mukwala muda mrefu tangu akiichezea Asante Kotoko ya Ghana, alisema mshambuliaji huyo ana kipaji cha pekee ila anahitaji kupewa nafasi tu kuthibitisha thamani aliyonayo.
Pluijm alisema anaamini Mukwala anakumbana na changamoto za kawaida ambazo wachezaji wengi hukutana nazo wanapohamia timu kubwa kama Simba.
Alisema wakati mwingine presha ya mafanikio kuto-kuelewana na mfumo wa timu mpya au ushindani mkali kutoka kwa wenzake kikosini vinaweza kum-fanya mchezaji kushindwa kufikia kiwango chake haraka kama inavyotarajiwa.
Pluijm anaamini uwezo wa Mukwala haujapungua na anachoona mshambuliaji huyo anatakiwa kujitu-ma mara mbili au tatu zaidi kuliko kawaida ili kufan-ikisha ndoto zake akiwa na Msimbazi.
“Mukwala ni mshambuliaji mzuri na naamini uwezo wake ni mkubwa. Hili ni jambo la muda tu kabla hajaanza kufunga mabao mengi. Muhimu ni kuwa na uvumilivu na kujituma zaidi, hasa katika mazingi-ra ya ushindani mkali ndani ya timu kama Simba.”
Maneno hayo yanadhihirisha imani ya Pluijm katika kipaji cha Mukwala na ushauri wake ni kwamba aongeze jitihada kwenye mazoezi na mechi.
Mukwala msimu uliopita alifunga mabao 14 akiwa na Asante Kotoko, anakabiliwa na ushindani mkali wa namba mbele ya Leonel Ateba, ambaye pia ame-funga mabao mawili.
Pluijm alisema ili kufanikiwa timu yenye mashabiki wengi na matarajio makubwa kama Simba, “ana-takiwa kubadilisha hali ya kushindwa kuwa motisha. Wakati mwingine inabidi kufanya kazi mara tatu hadi nne zaidi ya kawaida.”