Kanali Doumbouya ametangaza uamuzi huo wakati nchi hiyo ya Afrika Magharibi iliyokabiliwa na mapinduzi ikiashiria hatua za kuimarisha zaidi mamlaka ya vikosi vya kijeshi ambavyo tayari vina nguvu kubwa.
Kiongozi huyo wa kijeshi mnamo mwezi Januari pia alijipandisha cheo hadi kuwa Kanali mwezi Januari huku akiweka wazi kuwa serikali yake ya kijeshi haitatimiza ahadi yake ya kurudisha mamlaka kwa raia watakaochaguliwa ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Doumbouya, mwenye umri wa miaka 43, aliingia madarakani kwa nguvu mnamo Septemba mwaka 2021 kwa kumpindua aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Alpha Conde, ambaye alikuwa amempa cheo cha kanali mkuu wa kikosi maalum cha kijeshi kilichopewa jukumu la kumlinda mkuu huyo wa nchi dhidi ya mapinduzi ya aina hiyo.
Soma Pia: Milio ya risasi yasikika karibu na Ikulu ya Guinea
Katika amri iliyotangazwa siku ya Ijumaa jioni, Doumbouya ambaye wafuasi wake wamekuwa wakimsihi agombee urais baada ya serikali ya kijeshi itakapoacha hatamu alitunukiwa Tuzo ya juu ya Kitaifa ya Colratier, ambayo ni ya daraja la juu kabisa nchini humo. Heshima hiyo ni kutokana na juhudi zake za mara kwa mara za kukuza mshikamano wa kijamii na ushirikiano miongoni mwa watu wa Guinea.
Doumbouya aliyejima madaraka mapya ya Jenerali Mkuu ni mmoja wa maafisa kadhaa walionyakua mamlaka kwenye nchi za Afrika Magharibi angu mwaka 2020,sawa na viongozi wenzake wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger.
Kiongozi huyo wa kijeshi wa Guinea Mamadi Doumbouya, anaendeleza msako dhidi ya wapinzani, ambapo viongozi wengi wa upinzani wamewekwa kizuizini, wengine wamefikishwa mahakamani huku baadhi yao wakilazimika kuikimbia nchi.
Serikali ya kijeshi imepiga marufuku maandamano na hatua za vikosi vya usalama za kuyazuia maandamano yasiyoidhinishwa zimesababisha vifo vya watu kadhaa, kulingana na mashirika ya haki na mashirika ya kiraia.
Vyama vitatu viliwekwa chini ya uangalizi na vyama vingine 53 vilifutiwa usajili wake mnamo mwezi Oktoba katika kile serikali ya kijeshi ilichokiita “opereshi ya kuisafisha nchi kisiasa” kulingana na waraka rasmi ulioonekana na shirika la habari la AFP.
Soma Pia: Gabon, Guinea ya Ikweta zachuana mbele ya ICJ
Wizara ya mambo ya ndani ya Guinea, imesema kwenye ripoti yake kwamba, kati ya vyama 211 vilivyosajiliwa, vyama 53 vimefutwa, na vingine 54 vimesimamishwa kwa muda wa miezi mitatu huku vyama 67 vikiwekwa “chini ya uangalizi” kwa miezi muda wa mitatu ambapo vinaweza kusimamishwaau kufutwa endapo vitapatikanakuwa vimekiuka sheria za nchi.
Miongoni mwa vyama vilivyowekwa chini ya uangalizi ni vyama vitatu vikuu vinavyopinga utawala wa kijeshi, kikiwemo chama cha Rally of the Guinean People (RPG) kinachoongozwa na rais wa zamani wa kiraia Alpha Conde, ambaye alipinduliwa kwenye mapinduzi ya mwaka 2021.
Viongozi wa vyama vyote hivyo vitatu wamekimbilia uhamishoni.
Licha ya rasilimali zake nyingi za asili, Guinea bado ni taifa masikini. Nchi hiyo imetawaliwa na serikali za kimabavu na pia za kidikteta kwa miongo kadhaa.
Chanzo: AFP
Mhariri: Suleman Mwiru