Hamza: Nimejua ukubwa wa Simba

KITENDO cha mashabiki wa Simba kuliimba sana jina la beki wa kati wa timu hiyo, Abdulrazak Hamza, kimemmfanya beki huyo kushtuka na kubaini ana kazi kubwa ya kufanya ili kuendelea kulinda heshima aliyopewa tangu ajiunge na Wekundu hao.

Beki huyo alikosekana katika mechi kadhaa kutokana na kuumia na kuzua mjadala kwa mashabiki, kitu kilichomfanya Hamza akiri  amejifunza na kujua ukubwa wa majukumu aliyonayo na kuongeza nidhamu, kujituma katika majukumu yake.

Mwanaspoti lilimuuliza Hamza, anachukuliaje mashabiki wanaoumizwa kukosekana kwake uwanjani, alijibu: “Imenifunza kuongeza nidhamu, utulivu na kutokuchoka kujifunza maarifa kila wakati, pia inanipa presha kuona nachukuliwa kwa uzito.

Aliongeza: ”Kabla sijaumia nilikuwa nachukulia nafanya majukumu yangu kawaida, sikuwahi kujua ninachukuliwa kwa ukubwa, imenisaidia kutojisahau na kujiona nina kazi ngumu kulinda kiwango changu.”

Related Posts