Wadau wamvaa Mdoe | Mwanaspoti

TUKIO la mwamuzi wa kati, Omar Mdoe aliyechezesha pambano la Mashujaa na Simba na kuonekana aki msukuma Yusuf Dunia wa timu wenyeji wa mchezo huo wa Ligi Kuukatika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Mashujaa limewaibua wadau na kutoa maoni tofauti.

Mdoe alionekana kufanya tukio hilo akiwa katika harakati za kumtuliza Dunia aliyeonakana kulalamika kwa kuonekana kutokubaliana na maamuzi ya mwamuzi huyo kwa kupuliza kipyenga ikiwa ni faulo iliyoelekea upande wao baada ya Joshua Mutale kufanyiwa madhambi.

Kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar na Gwambina, Mohamed Badru alisema ni sawa mwamuzi kuwa mkali lakini anatakiwa kuwa na kiasi.

“Mwamuzi naye ni binadamu kuna muda naye damu inachemka lakini sidhani kama Mdoe alikuwa na nia yoyote mbaya zaidi ni kama alihitaji kumuonya kwa vitendo mchezaji wa Mashujaa na wala hakuwa na dhamira mbaya,” alisema kocha huyo. 

Mchezaji wa zamani na mchambuzi wa soka, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ naye alionekana kushangazwa na tukio la Mdoe na kuamua kuandika ujumbe katika mitandao ya kimaii kisha akiambatanisha na video ya tukio.

“Nifikishieni Salamu kwa Mwamuzi wa mechi ya leo ya Sokwe (Mashujaa) vs Lion (Simba) kwamba hii sio silaha yake, silaha yake ni kadiiii,” ujumbe ulisomeka.

Alipotafutwa mwamuzi mkongwe Soud Abdi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi alisema; “Kimaadili siruhusiwa kuongea kuhusu hilo tukio lakini ipo kamati ambayo kazi yake hufanya mapitio hivyo wanaweza kutazama na kuona kama hakufanya sahihi au laa.”

Related Posts