Sababu Fountain v Alliance kusogezwa mbele

MCHEZO kati ya Fountain Gate Princess na Alliance Girls uliopangwa kuchezwa kesho Novemba 5 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma umesogezwa hadi keshokutwa Novemba 6 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mkoani Manyara.

Inaelezwa sababu ya mechi hiyo kusogezwa mbele ni kutokana na Fountain Gate kuomba mechi ichezwe Babati hivyo imesogezwa ili kupata muda mzuri wa kujiandaa.

Hii inatokana na Fountain Gate Princess kwa sasa kuwa chini ya timu ya Fountain Gate ya wanaume na hivyo haitakuwa chini ya Akademi ya Dodoma.

Akizungumza juu ya ratiba hiyo, kocha wa Fountain, Camil Mirambo alisema Novemba mosi waliwasili Babati na wamepata muda wa siku tatu wa kujiandaa.

“Ni kweli kwa sasa tutakuwa Babati mkoani Manyara baada ya kuwa chini ya Fountain Gate na tunashukuru tuliwasili salama na hadi sasa hakuna majeraha yeyote,” alisema Mirambo.

Related Posts