JWTZ watoa msaada kwa watoto yatima waliopoteza wazazi vitani Congo

Walinda amani wa JWTZ chini ya MONUSCO wanaohudumu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametoa msaada kwa Watoto yatima ambao wamepoteza Wazazi wao kutokana na migogoro inayoendela Nchini humo.

Kamanda wa Kikosi cha 11 cha Tanzania Luteni Kanali Verdasto Ernest Kikoti ameongoza zoezi la utoaji msaada huo ambapo amesema pamoja na jukumu la msingi walilonalo la ulinzi wa amani DRC, wameguswa kuwasaidia Watoto yatima kwasababu yanapotokea machafuko wanaothirika ni Watoto na Wanawake hivyo wataendelea kuwasaidia kwa kuwapa mahitaji kwa kadri watakavyoweza .

Kiongozi wa kituo cha Watoto yatima cha Mungu ni Mwema kilichopo Boikene Mjini Beni, Masika Kombi Prisca, anewashukuru Walinda amani wa JWT kwa misaada hiyo na kusema kituo kilikuwa na changamoto ya magodoro, chakula, vyombo vya kupikia, vifaa vya Wanafunzi na nguo na kwamba msaada umewafikia wakati mwafaka.

Walinda amani hao wametoa magodoro, sabuni, chakula, madaftari, kalamu, mafuta ya kula na vifaranga vya kuku.

Related Posts