SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBU YA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombu ya kutolea huduma za afya ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za kimkakati ili kuendelea kutoa huduma kwa Wananchi.

Mhe. Katimba amesema hayo katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe.Tumaini Bryceson Magessa Mbunge wa Jimbo la Busanda alieyeuliza Je, lini Serikali itajenga vituo vya afya Kata za Lwanzasa, Nyakagomba na Magenge – Busanda.

Amesema hadi kufikia Septemba, 2024 Serikali ilikuwa imekamilisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya 898 ambavyo vinatoa huduma ngazi ya kituo cha afya ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji wa dharura vikiwemo vituo vya afya vya Bukoli na Nyakagwe kwa thamani ya shilingi milioni 400 katika Jimbo la Busanda.

“Serikali itaendeea kujenga vituo vya afya katika Kata za kimkakati kote Nchini zikiwemo Kata zitakazo kidhi vigezo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita kadiri fedha zitakavyopatikana.”

Related Posts