PICHA :Mazishi ya Jenerali mstaafu David Musuguri nyumbani kwake katika Kijiji cha Butiama

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko amewaongoza wananchi na waombolezaji katika mazishi ya  Jenerali mstaafu David Musuguri nyumbani kwake katika Kijiji cha Butiama, wilaya Butiama mkoani Mara

Biteko ambaye amemwakilisha Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza waombolezaji wakiwemo viongozi wa Serikali na Wanasiasa katika tukio hilo lililoendeshwa kwa taratibu za Kidini na Kijeshi.

Jenerali Musuguri alizaliwa mwaka 1920, na kufariki Dunia October 29, 2024 katika Hospitali ya Rufani ya Kanda Bugando Mwanza, alikokuwa akipatiwa matibabu

Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Dini na Siasa waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri wa Ulinzi Strogomena Tax, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Patrick Chandi, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro, Naibu Waziri Katiba na Sheria Jumanne Sagini na Askofu wa Kanisa la Roman Katoliki mkoani Mara Michael Msonganzila na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jacob Mkunda.

Related Posts