Wizara ya Nishati yakamilisha maandalizi kuelekea Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio ameongoza kikao kazi cha mwisho cha maandalizi ya ushiriki wa Wizara hiyo katika Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika utakaofunguliwa rasmi Novemba 05, 2024 Jijini Cape Town – Afrika ya Kusini.

Kikao kazi hicho kilichohusisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake kimefanyika Novemba 04, 2024 ili kuhakikisha ushiriki wa Wizara katika Mkutano huo unaleta matokeo tarajiwa.

Wizara ya Nishati inashiriki Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika 2024 kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya nishati.

Miongoni mwa fursa zitakazozungumziwa na Wizara ya Nishati ni pamoja na uwekezaji katika vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia, miundombinu ya mafuta na gesi, miradi ya nishati jadidifu na viwanda vya petrokemikali.

Kwa ufupi, Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika unaleta pamoja washiriki zaidi ya 5000 kutoka ndani na nje ya Afrika.

Mkutano huo unaambatana na maonesho yanayofanywa na kampuni mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi) Dkt. James Mataragio akiongoza kikao cha maandalizi kuelekea Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika utakaofunguliwa rasmi Novemba 05, 2024 Jijini Cape Town – Afrika ya Kusini.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio akiongoza timu ya wataalamu katika maandalizi ya mwisho kuelekea Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika 2024

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio (katikati) akiongoza kikao kazi cha maandalizi ya ushiriki wa Wizara katika Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika utakaofunguliwa Novemba 05, 2024 Capetown Afrika ya Kusini.

Timu ya wataalamu chini ya uenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio wakati wa kikao cha maandalizi kuelekea Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika 2024

Related Posts