Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiondoa kitambaa tayari kuzindua Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akikagua vitanda mara baada ya kuzindua Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Kamanda Kikosi 825 KJ, Mtabila Luteni Kanali Patrick Ndwenya,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzinduliwa Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Na.Alex Sonna_KASULU
MKUU wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, amezindua Mahanga 15 ya Vijana katika kikosi cha Jeshi 825 KJ Mtabila kilichopo Kasulu mkoani Kigoma huku akiishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika vikosi vya JKT.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mahanga hayo Bregidia Jenerali Mabena alisema kila mwaka serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vikosi.
Bregidia Jenerali Mabena,alisema kuwa mahanga hayo yana uwezo wa kuchukua wanafunzi 100 kwa kila hanga moja na kufanya ongezeko la vijana 1500 kwenye kikosi hicho.
“Mahanga haya yanaleta maana kubwa kwa sababu lengo la mafunzo haya kwanza ni kuwafikia vijana wote wa kundi la lazima waliomaliza kidato cha sita na vijana wengine kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ili kuweza kuwapata vijana wote kuhudhuria mafunzo ya uzalendo ,kulipenda Taifa lao,kuwaweka pamoja na kuondoa tofauti dhidi yao .
Aidha ameishukuru serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo ambapo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake wa wameendelea kupata fedha ambazo wamekuwa wakizielekeza kwenye vikosi vya JKT kuhakikisha wanakwenda kuongeza idadi na hatimaye kuchukua vijana wengi kwa wakati mmoja na kuwaweka pamona.
“Nchi yetu ni kubwa ina watanzania zaidi ya milioni 60 kwa hiyo vijana wa kitanzania wamezaliwa maeneo mbalimbali hivyo unapowaweka pamoja kuwaelekeza utamaduni wa nchi yao inakuwa ni jambo jema sana”alisema na kuongeza kuwa
“Niendelee kuipongeza Serikali lakini zaidi niwapongeze makamanda vikosi kwani wameweza kuielewa vyema ile nia thabiti ya Makao Makuu ya JKT,wizara ya Ulinzi na JKT na Taifa kwa ujumla la kuwaweka vijana hao pamoja na kutekeleza maagizo hayo kwa vitendo.”
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu JKT katika kikosi cha 825 KJ Amina Singano alisema kama vijana,watayatunza majengo hayo ili yaweze kufumu kwa muda mrefu.