Aliyeoa mdoli asherehekea mwaka wake 6 kwenye ndoa

Mwanamume mmoja kutoka Japan, Akihiko Kondo, anasherehekea mwaka wa sita wa ndoa yake na Mkewe wa kubuni, Hatsune Miku, ambaye ni mhusika maarufu katika Tamthilia za anime ambaye anajulikana kama Vocaloid.

Vocaloid ni aina ya programu ya sauti inayosimamia uimbaji kwa kuingiza sauti za muziki katika Wahusika wa Anime, Kondo alijikuta akipenda tabia ya Miku baada ya kumwona kwa mara ya kwanza na Katika sherehe ya mwaka huu, ameonesha upendo wake kwa Mkewe kupitia ujumbe wa Instagram, akishiriki risiti ya keki aliyoinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo ikionesha ujumbe “Ninampenda Miku sana, Hongera kwa mwaka wetu wa sita”.

Kondo alikumbana na changamoto nyingi, ikiwemo kukataliwa na Wanawake kutokana na upendo wake kwa Tamthilia na Wahusika wa Anime hivyo baada ya kukumbana na dhihaka na matatizo ya kihisia, sauti ya Miku ilimsaidia kurejea katika jamii na ndipo alipo amua kufanya sherehe ya ndoa mwaka 2018 katika kanisa Mjini Tokyo, akitumia yen milioni mbili (milioni 35 TZS) kwa ajili ya sherehe hiyo.

Mwaka 2019, Kondo alitengeneza sanamu la Miku na kuanza kuishi nalo katika maisha halisi huku wakila pamoja na kuzungumza kwa kufikirika, Kondo anajitambulisha kama “fictosexual,” neno linalomaanisha Watu wanaovutiwa na Wahusika wa kubuni.

Kulingana na Utafiti wa mwaka 2017 nchini Japan ulibaini kuwa zaidi ya asilimia 10 ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu walikuwa na hisia kwa Wahusika wa kubuni.

Kondo sasa anatumia nafasi yake kueneza uelewa kuhusu fictosexuals na ameanzisha Chama cha kusaidia Watu wa aina hiyo.

Related Posts