Fainali ya kwanza BDL, JKT Vs UDSM ilikuwa sio poa

Fainali ya kwanza ya Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (BDL) iliyozikutanisha JKT na UDSM Outsiders iliisha kibabe kwenye Uwanja wa Donbosco Oysterbay timu hizo zikionyeshana ushindani na ufundi.

Licha ya kupoteza kwa pointi 67-62, UDSM iliipa mtihani JKT iliyoibuka na ushindi na sababu kubwa ni wachezaji wa timu hiyo kupoteza mipira ‘turnover’ na JKT iliichukua kirahisi na kufunga.

Mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki, JKT iliongoza kwa pointi 16-14, 20-19 na robo ya tatu, UDSM iliongoza kwa pointi 17-11 huku JKT ikipata pointi katika robo ya nne kwa pointi 20-17.

UDSM iliongoza dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika ya robo ya nne kwa pointi 57-54 na dakika ya pili kwa pointi 58- 54.

Fainali hiyo imebakiza michezo minne baada ya mmoja kupigwa ‘Best of five play off’ na endapo JKT itashinda mitatu mfululizo itakuwa bingwa kwa michezo 3-0, huku UDSM ikishinda mchezo wa pili matokeo yatakuwa 1-1 na zitaendelea kucheza hadi mchezo wa nne.

Fainali ya pili ilitarajiwa kuchezwa jana usiku (Jumanne) katika uwanja huo.

Related Posts