Waliotuhumiwa kumuua dereva wa bodaboda wafikishwa kortini

Morogoro. Wakazi wanne wa wa Ifakara wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya mkoani Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya dereva wa bodaboda, Shabani Mhawile.

Washitakiwa hao ni Denis Swai maarufu kama Nkane, (34), Athumani Mpango (38), Musa Bushiri (28) na Alhaji Likwaya (32).

Akiwasomea shitaka hilo la mauaji mahakamani hapo, Wakili wa Serikali, Simon Mpina mbele ya hakimu Regina Futakamba amedai kuwa, washtakiwa hao walitenda kosa hilo Septemba 5 2024, katika kambi ya uvuvi Senga.

Amedai kuwa washitakiwa kwa pamoja   baada ya kutekeleza mauaji hayo, walikwenda kumtupa bodaboda huyo kwenye Pori la Akiba Kilombero maeneo ya Ipatilo Kata ya Minepa.

Wakili wa Serikali, Mpina amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

 Baada ya kusomewa shitaka hilo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na Mahakama hiyo kukosa mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi za mauaji, hivyo walirudishwa rumande hadi Novemba 18 mwaka huu kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana kisheria.

Related Posts