TBT yabeba ubingwa Kigoma | Mwanaspoti

TBT imetawazwa mabingwa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Kigoma, baada ya kuifunga Wavuja jasho kwa pointi 62-61, katika fainali ya tano iliyofanyika Uwanja wa Lake Side.

Fainali hiyo ilichezwa kwa timu kucheza mara saba ‘best of seven play off’, TBT ilishinda michezo 5-1.

Katika mchezo wa kwanza, TBT ilishinda kwa pointi 52-50, 78-67 na wa tatu Wavuja Jasho ilishinda 87-67.

TBT iliedelea ushindi kwa kushinda fainali ya nne kwa pointi 72-60 na mchezo wa tano ikashinda 62-61.

Katika mchezo wa mwisho wa fainali hiyo, Evansi Evodi ‘Kiboko’ wa TBT alifunga pointi 20, huku george Magasa wa Wavuja Jasho akifunga 15.

Related Posts