Eagles yatinga fainali MRBA | Mwanaspoti

EAGLES imetinga fainali baada ya kuifunga Young Profile kwa pointi 73-51, katika nusu fainali ya pili ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mwanza (MRBA), katika uwanja wa Mirongo.

Katika mchezo huo, Eagles ilishinda pointi 73-51 baada ya awali kushinda 73-72 kwenye mchezo wa pili kati ya mitatu ya ‘best of three play off, hivyo kuwa na ushindi wa jumla wa 2-0.

Katika mchezo huo Young Profile iliongoza robo mbili za kwanza kwa pointi 20-14 na 13-10, huku robo ya tatu Eagles ikipindua ubao na kuongoza kwa pointi 27-12 na robo ya tatu ikapata pointi 22 na kuifanya iibuke na ushindi wa pointi 73-51.

Timu hiyo inasuburi mshindi kati ya Profile na Planet na  katika mchezo wa kwanza, Planet ilishinda kwa pointi 58-48.

Related Posts