MAPATO YAPAA KISHAPU, MADIWANI WAANIKA CHANGAMOTO ZA BARABARA, ZAHANATI, SHULE


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Willium Jijimya akizungumza kwenye kikao cha madiwani na wataalam kikao cha kupokea taarifa za utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo robo ya kwanza 2024/2025 kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Picha na Sumai Salum


Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Emmanuel Johnson akizungumza kwenye kikao cha madiwani na wataalamu kikao cha kupokea taarifa za utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo robo ya kwanza 2024/2025 Novemba 5,2024 kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo.

Na Sumai Salum-Kishapu

Taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga, zimeonyesha mafanikio ya kupanda kwa mapato, kutokana na ukusanyaji mzuri wa mapato unaozingatia sheria, kanuni, na taratibu.

Katika kikao cha Novemba 5, 2024, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, madiwani wa kata mbalimbali walipowasilisha taarifa za maendeleo ya kata zao, wamesema kuwa licha ya mafanikio hayo, bado wanakabiliana na changamoto kubwa za miundombinu na huduma za jamii.

Diwani wa Kata ya Bubiki, Mhe. James Kasomi, ameeleza kuwa wamefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Milioni 11, ingawa kata hiyo inakumbwa na matatizo ya uchakavu wa madarasa katika Shule ya Msingi ya Bubiki, ukosefu wa nyumba za walimu katika Shule ya Msingi Ushirika, pamoja na uhitaji wa kumaliza ujenzi wa zahanati.

Kwa upande mwingine, Diwani wa Kata ya Masanga, Mhe. Enock Reuben, amebainisha kuwa kata hiyo imekusanya zaidi ya Shilingi Milioni 14 katika robo hii ya kwanza ya mwaka 2024/2025. Hata hivyo, ameeleza kwamba mradi wa maji safi wa Masanga-Ndololeji, uliotakiwa kukamilika mwezi Agosti 2024, umechelewa kukamilika na hivyo kuathiri huduma za maji kwa wananchi wa kata hiyo.

Taarifa za Kata ya Ngofila, zilizowasilishwa na Diwani Mhe. Nestori Ngude, zilionyesha kuwa kata hiyo inakabiliwa na changamoto za upungufu wa vyumba vya madarasa katika baadhi ya shule za msingi, uhaba wa madawati, na matatizo ya miundombinu ya vyoo. Aidha, mradi wa maji safi na salama unakumbwa na ucheleweshaji,na ujenzi wa zahanati ya Inolelo bado haujakamilika.

Wakati huo, Diwani wa Kata ya Kiloleli, Mhe. Edward Manyama, amezungumzia umuhimu wa kufanya ukarabati wa mapema wa barabara, akisisitiza kwamba hatua hiyo itasaidia kupitisha masanduku ya kupigia kura kwa usalama kipindi cha uchaguzi, hasa wakati wa mvua.

Akijibu hoja hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Bw. Emmanuel Johnson, amewataka wakuu wa idara kuwa makini katika kufuatilia changamoto zilizobainishwa katika taarifa za kata na madiwani ili ziweze kushughulikiwa haraka.

Ametoa wito kwa madiwani na wananchi kuipa kipaumbele zahanati, na kuahidi kuwa serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara.

“Kwa bahati nzuri, tunaanza mwaka wa fedha, hivyo niwashauri waheshimiwa madiwani na wananchi tuzipe zahanati zetu kipaumbele na kuzitengea fedha ili kumaliza ukarabati haraka iwezekanavyo, kama vile zahanati za Bubiki na Inolelo kata ya Ngofila,” amesema Bw. Johnson.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeongeza bajeti kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara, ambapo baadhi zitajengwa kwa kiwango cha lami, huku pia wakandarasi wakianza kazi hivi karibuni.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kishapu, Peter Mashenji, amewataka watendaji wa halmashauri hiyo kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia changamoto hizo ili kujibu hoja za wananchi na kuhakikisha maendeleo ya kata yanapata kasi ya utekelezaji.

Katika ujumla, kikao hicho kimejikita katika kufuatilia maendeleo ya miradi na changamoto zinazokabili maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kishapu, huku viongozi wakihimiza ushirikiano wa pamoja kati ya serikali, madiwani, na wananchi ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha huduma za kijamii.


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Petter Francis Mashenji akizungumza kwenye kikao cha uwasilishwaji taarifa za shughuli mbalimbali za maendeleo ya kata kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa halmashauri hiyo


Diwani wa kata ya Mwamalasa Mhe.Bushi Salum akizungumza kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa za utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo robo ya kwanza 2024/2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo Novemba 5,2024

Diwani wa Kata ya Ngofila Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Nestory Ngude akiwasilisha taarifa ya kata hiyo kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa za utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Diwani wa kata ya Kiloleli Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Edward Manyama akichangia hoja ya ukarabati wa miundombinu ya barabara kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa za utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Diwani wa kata ya Songwa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Abdul Ngolomole akichangia hoja ya ukarabati wa miundombinu ya barabara kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa za utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa halmashauri hiyo.


Diwani wa Kata ya Masanga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Enock Reuben akiwasilisha taarifa ya kata hiyo kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa za utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Diwani wa kata ya Bubiki Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. James Kasomi akisoma taarifa ya utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo ya kata hiyo ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye kikao kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa halmashauri hiyo.


Diwani wa kata ya Ndololeji Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Mohamed Amani akichangia hoja ya kutokamilika kwa wakati mradi wa maji safi kwa wakati katani kwake kwenye kikao cha uwasilishaji taarifa za utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Diwani wa kata ya Bubiki Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.James Kasomi akisoma taarifa ya utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo ya kata hiyo ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye kikao kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa halmashauri hiyo.








Wataalamu mbalimbali wa halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakifuatilia kikao cha uwasilishaji taarifa za maendeleo ya kata robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri Novemba 5,2024.




Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakifuatilia kikao cha uwasilishaji taarifa za maendeleo ya kata robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 katika ukumbi wa halmashauri Novemba 5,2024

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Shija Ntelezu akifuatilia taarifa za maendeleo ya kata robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye kikao kilichohusisha madiwani na wataalam wa Halmashauri kikao kilichofanyika Novemba 5,2024 katika ukumbi wa halmashauri hiyo

Related Posts