Vijana wa Kitanzania Kuwezeshwa kupitia Vodacom Youth Base (VYB), kuongeza fursa katika za kidijitali. – MWANAHARAKATI MZALENDO

Meneja wa Bei na Bidhaa kutoka Vodacom Tanzania, Ipyana Mwankemwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya VYB Balaa! Mtu ni Connection! ambapo vijana wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 28 wanapata nafasi ya kufaidika na vifurushi mbalimbali kutoka mtandao huo. Uzinduzi huu uliopambwa na burudani kemkem ulifanyika tarehe 24 Oktoba 2024 Don Bosco Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam: Vodacom Tanzania Plc imezindua Vodacom Youth Base (VYB), kampeni bunifu inayolenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 na 28, ili waweze kufikia mtindo wa maisha wa kidijitali. Jukwaa la Vodacom Youth Base (VYB) linakuja na faida mbalimbali ikiwemo, jumbe fupi za bure (SMS), punguzo la vifaa vya kielectroniki kama vile simujanja na vifurushi vya gharama nafuu na miamala bila makato.

Katika ulimwengu wa kidijitali unaobadilika kwa kasi, ambapo upatikanaji wa teknolojia ni muhimu ili kufungua fursa, VYB imezinduliwa ikiwa ni jukwaa linalovuka  mawasiliano ya simu. Kwa kujiunga na VYB, vijana wataweza kupata huduma za mawasiliano kwa bei nafuu pamoja na bidhaa nyingine  muhimu kama ofa za kipekee, fursa za kujifunza na kuongeza  ujuzi, na uwezo wa kuungana na wenzao pamoja na wakufunzi ambao watawasaidia kujiandaa kwa maisha yao ya kujitegemea.

Kauli mbiu ya kampeni hii “Mtandao Wako ni Thamani Yako,” inadhihirisha kuwa mawasiliano bora, upatikanaji  wa intaneti na fursa za ukuaji vinaboresha uwezo wa vijana kufanikiwa katika uchumi wa kidijitali wa leo. Kila mteja wa Vodacom ndani ya umri tajwa ataunganishwa moja kwa moja, bila kuhitaji kuchukua hatua zozote za ziada ili kuhakikisha upatikanaji  wa faida hizi.

Kwa kutumia VYB, vijana wa Kitanzania watapata zaidi ya faida za mawasiliano, watapata zana za kujenga taaluma, mipango ya ukuaji na fursa za mtandao zinazokusudia kuwapa uwezo wa kufanikiwa na kujitegemea. Lengo ni kuhakikisha kwamba kila kijana, bila kujali uwezo wa kifedha, anaweza kushiriki katika mabadiliko ya kidijitali yanayofanyika duniani.

“Tunatambua uwezo mkubwa ulio ndani ya vijana wa Tanzania; wao ni wabunifu, wajasiriamali, viongozi, na waleta mabadiliko, hivyo wanastahili zana zinazounga mkono ndoto zao,” alisema Brigita Stephen, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom. “Kupitia VYB, tunahakikisha kwamba vijana si tu wanaunganishwa bali pia wanapata rasilimali wanazohitaji ili kufanikiwa katika uchumi wa kidijitali, kwa sababu kufanikiwa kwa vijana hawa, ni kufanikiwa kwa taifa  zima.”

Kampeni ya VYB imezinduliwa katika kituo cha mafunzo ya ufundi cha Vijana cha Don Bosco, ambacho kinajulikana kwa kujitolea kwake katika uwezeshaji na maendeleo ya vijana nchini. Akizungumza kuhusu umuhimu wa uzinduzi huu.

Maureen Njeri, Meneja Mkazi wa  Mdundo aliipongeza Vodacom  kwa hatua hii na kusema kwamba Ushirikiano wa Mdundo na Vodacom unathibitisha kauli mbiu ya Vodacom ‘Pamoja Tunaweza,’ “Tangu mwaka 2020, tumekuwa tukifanya kazi pamoja na tutaendelea kufanya kazi pamoja na Vodacom katika kuleta burudani bora kwa vijana. Yajayo yanafurahisha, kaa mkao wa kula,” alisema Maureen.

Alidadavua kwamba VYB inawawezesha wateja wa Mdundo kupata urahisi na uhalali wa kupata Top Dj Mixes katika miziki ya Bongo Flava, Singeli, Qaswida, Taarab, Gospel, Afro beats, Amapiano huku akiongeza kwamba kila siku Mdundo wanatoa Dj mixes mpya ambazo zinaweza kupakuliwa moja kwa moja kwenye simu kwa kutumia kifurushi maalum cha VYB.

“Kama Mdundo, tunahamasika kufanya kazi na na Wasanii Pamoja na watumbuizaji hapa nchini huku tukiwapa fursa ya kupata hela kutokana na bidi zao, Mdundo ina watumiaji hai takribani 31.8 milioni duniani huku hapa nchini wakiwa ni 3.1 milioni kwa mwezi, tunalenga kutoa mirahaba yenye thamani yad ola 3.2 bilioni kwa wasanii wa Afrika kwa mwaka ujao,” alifafanua Maureen.

“Ili kuingia kwenye jukwaa, mteja yeyote wa Vodacom aliyesajiliwa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) na mwenye umri kati ya miaka 15 na 28 ataandikishwa moja kwa moja kwenye programu ili kuhakikisha mpito rahisi ili vijana waweze kufurahia faida za VYB,” alihitimisha Brigita.

 

MWISHO.

 

 

Related Posts

en English sw Swahili