Chuma Cha Chuma arejeshwa mahakamani kujua hatma ya dhamana yake

Kijana Ferdnand Ndikuriyo (27) maarufu kwa jina la Chuma Cha Chuma ambaye ni Raia wa Burundi, amerudishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo November 06,2024 kwa ajili ya kujua hatma ya dhamana yake.

Chuma kwa Chuma akikabiliwa na mashitaka ya kuishi Nchini Tanzania bila kibali.

Chuma ambaye ni Mkazi wa Mbezi Louis, Dar es salaam, alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swalo ambapo Wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji, Ezekiel Kibona, amedai Chuma alitenda kosa hilo September 18,2024 eneo la Upanga, Las Vegas Casino Wilaya ya llala Dar es Salaam na kwamba akiwa eneo hilo alibainika kuwepo Nchini bila kibali.

 

Baada ya kusomewa mashitaka yake Mshitakiwa huyo amekana kutenda kosa hilo huku Wakili wake akidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo kuiomba Mahakama iwapangine tarehe nyingine ya kutajwa.

Mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi leo.

Related Posts