Latra Morogoro yasisitiza matumizi ya sheria za usalama barabarani mwisho wa mwaka

Afisa mfawidhi wa Mamlaka ya uthibiti wa usafiri ardhini (LATRA) Mkoa wa Morogoro Andrew Mlacha amesema ajali nyingi zinazotokea barabarani zinasababishwa na makosa ya kibinadamu.

Mlacha amesema hayo wakati akizungumza na Madereva wa kampuni ya Abood wakati wakipatiwa mafunzo maalum ya kukumbushwa kutii na kufuata Sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

Amesema Madereva wanatakiwa kukumbushwa mara Kwa mara Sheria za usalama barabarani ili kuthibiti matukio hayo ambapo ameipongeza kampuni hiyo Kwa kutuo mafunzo hayo.

Mlacha ameongeza Kwa kusema kuwa hata hivyo kutakuwa na mitihani Kwa Madereva wote ili kupima uwezo wao na kusajiliwa hivyo basi mafunzo hayo yamekuja muda muafaka na yataleta tija.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya Abood Moris Masala amesema mafunzo hayo ni mikakati ya kuboresha huduma Kwa abiria ambapo yatakuwa endelevu Madereva wote kampuni hiyo.

Amesema baada ya Madereva hao pia wahudumu watapatiwa mafunzo ya huduma Kwa wateja kwani nao ni sehemu ya huduma ambazo abiria anatakiwa kuzipata muda wote Katika safari.

Naye Mkufunzi wa Mafunzo John John amesema licha ya kuwakumbusha matumizi ya alama za barabara lakini pia wanakumbushwa kuendesha Kwa tafadhari na kujihami.

Nao baadhi ya Madereva hao wakipatiwa mafunzo wamesema mara nyingi wamekuwa wakikiuka Sheria za usalama barabara Kwa kutojua hivyo mafunzo hayo yatakwenda kuboresha utendaji kazi wao.

Related Posts