WAKURUGENZI WAELEKEZWA KUFANYA MSAWAZO WA WALIMU

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafanya msawazo wa walimu kwa kuzingatia bajeti ndani ya Halmashauri ili kutengeneza uwiano sawa kwa shule zote za mijini na vijijini.

Mhe. Katimba ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wanchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la Mhe. Emmanuel Mwakasaka mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini aliyetaka kujua serikal inampango gani wa kuhakikisha walimu wanakaa vijijini badala ya kukimbilia Mjini.

Akijibu swazi hilo Mhe. Katimba amesema “serikali inatambua kuna changamoto ya walimu kupenda kukaa mijini na kwaniaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI kuwaagiza wakurugenzi wote waweze kuhakikisha kwa kuzingatia bajeti wanaweza kufanya msawazo wa walimu ili kutengeneza uwiano na kuondoa maeneo ambayo yana walimu wengi zaidi na kupelekea maeneo ambayo niya vijijini ambapo hamna walimu kwahiyo wakurugenzi wafanye kazi hiyo” amesema

Awali akijibu swali la Mhe. Mwakasaka linalohusu upungufu wa walimu katika baadhi ya maeneo nchini amesema amesema tayari serikali imetangaza ajira na mwaka huu baada ya mchakato wa ajira watapangiwa vituo vya kazi.

Related Posts