64 wahukumiwa kwenda jela ,kosa la kwenda nchini Afrika Kusini (Kuzamia) kinyume cha sheria

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu watu 64 kwenda jela miezi sita ama kulipa faini ya Shilingi Elfu Arobaini baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kwenda nchini Afrika Kusini (Kuzamia) kinyume cha sheria.

Haya hivyo, watu hao wamefanikiwa kukwepa adhabu ya kutumikia kifungo hicho baada ya kulipa faini hiyo ya Elfu Arobaini.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki ambapo walisomewa makosa yao Wakili wa Serikali, Ezekiel Kibona akisaidizana na Grace Nyarata alidai washitakiwa wote wanakabiliwa na kosa moja.

Waliohukumiwa ni Abdallah Ramadhani(29), Abdul Rajabu (49), Abdul Lusambi (23), Abdulrahman Mtimbe(38), Abubakar Feruz (28), Abubakar Kitemba(29), Abuu Kabaga(28), Adam Kiselekela(31).

Wengine ni Adam Mkumba(30), Akida Ally(24), Ally Maduka(24), Ally Ally(42), Ally Mpene(28), Ally Mohamed(36), Amary Hemed(27), Ashrafu Matata(30), Athuman Ramadhan(18) na wengine 47.

Katika mashtaka yao inadaiwa kuwa Oktoba 29,2024 washitakiwa wakiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikutwa wameondoka kuelekea Afrika Kusini kwa tarehe tofauti bila kufata taratibu na sheria za uhamiaji za kuondoka nchini.

Baada ya kusomewa shitaka hilo washitakiwa wote walikiri kutenda kosa hilo.

Baada ya kukiri Kibona aliwasomewa washitakiwa maelezo ya awali na kudai kuwa washirakiwa wote ni raia wa Tanzania ambao katika tarehe tofauti kupitia mipaka tofauti waliondoka nchini bila kibali.

Aliendelea kudai kuwa katika tarehe na majira tofauti washitakiwa walikamatwa Afrika Kusini kwa makosa mbalimbali likiwemo la kuwepo nchini humo kinyume cha sheria na bila kuwa na vibali.

Pia alidai Oktoba 29,2024 washitakiwa wote waliondolewa Afrika Kusini na kurudishwa Tanzania na katika tarehe hiyo baada ya kufika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere washitakiwa walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kuondoka nchini kinyume cha sheria.

Pia katika tarehe hiyo washitakiwa wote walifikishwa katika ofisi za uhamiaji na baadaye kuambiwa haki zao za msingi na kuanza kuhojiwa na wote walikiri kutenda kosa hilo.

Novemba 4,2024 washitakiwa wote walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa makosa yao yanayowakabili ambalo ni kuondoka nchini bila kufata sheria za uhamiaji za nchi zinavyoelekeza.

Baada ya maelezo hayo washitakiwa wote walikiri kuwa hoja hizo ni za kweli.

Kibona aliiomba mahakama iwape washitakiw adhabu kulingana na makosa wanayoshitakiwa nayo.

Pia washitakiwa waliiomba mahakama iwapunguzie adhabu na isiwape adhabu kali na kuahidi kuwa hawatorudia tena kufanya makosa hayo

Related Posts