WAZIRIย wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolfย Mkenda akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 6,2024 jijini Dodoma kuhusuย kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ย linalofanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
WAZIRIย wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolfย Mkenda,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa naย waandishi wa habariย kuhusuย kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ย linalofanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga, akizungumza na waandishi wa habariย kuhusuย kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifuย ย litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuuย Wizara yaย Elimu, Sayansi na Teknolojiaย Prof. Carolyneย Nombo,akielezea lengo laย kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifuย ย litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH ) Dkt.Amos Nungu,akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifuย ย litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Na.Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Samia Suluhu Hassan kuzindua Mfuko wa Mikopo wa kusaidia Ubidhaishaji na Ubiasharishaji wa ubunifu na teknolojia zinazobuniwa na vijana wa Kitanzania.ย
Dkt.Samiaย anatarajia kufanya hayo akiwaย mgeni rasmi katika Kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu linalofanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 6,2024 jijini Dodoma ย amesema kongamano hilo linatarajia kufanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4, 2024ย katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam linalokwenda na Kauli mbiu ya Kongamano kwa mwaka huu kuwa niโMatumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ununifu katika Kuhimili Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi na Kuchangia kwenye Uchumi Shindaniโ.
Prof.Mkendaย amesema Kongamano hiloย linalenga kuwaleta pamoja watafiti, wabunifu, na wadau kutoka sekta mbalimbali, ndani na nje ya nchi ili kujadili kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha mchango wa Sayansi, teknolojia na ubunifu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Prof.Mkenda amesema kuwaย Rais Dk.Samiaย atazindua rasmi mfuko wa mikopo wenye kianzio cha Shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya kusaidia ubidhaishaji na ubiasharishaji wa bunifu na teknolojia zinazobuniwa na vijana wa Kitanzania;
“Katika Kongamano hilo Rais Dk.Samia atakabidhi hundi yenye thamani ya sh.bilioni 6.3 kwa watafiti 19 katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo nishati safi ya kupikia, atawatambua na kutoa tuzo maalumu kwa wanasayansi na wabunifu ambao matokeo ya kazi zao yamechangia kuleta mabadiliko ya kiuhumi na kijamii, ndani na nje ya nchi,”amesema Prof.Mkenda
Aidha amesema kuwaย kabla ya hafla ya ufunguzi,ย Rais Samiaย ย atapata fursa ya kutembelea maonesho ili kujionea baadhi ya matokeo ya utafiti na ubunifu ambayo yamechangia katika kubadili mfumo wa kiuchumi na kijamii hapa nchini.
Pia Prof.Mkenda amesema kuwaย kupitia Kongamano hilo Serikali itapata michango ya kisera na kitaalamu ambayo itasaidia kuimarisha sera, mikakati, na juhudi nyingine zinazolenga kuimarisha mchango na mshikamano baina ya taasisi, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo katika kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kama nyenzo kuu ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania.
Hata hivyo Prof.Mkenda,amewaalika Watanzania wote pamoja na wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi, ndani na nje ya nchi, kushiriki Kongamano hilo.
โili kufanikisha na kufikia malengo yaliyokusudiwa, nitumie fursa hii kuwaalika Watanzania wote pamoja na wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi, ndani na nje ya nchi, kushiriki Kongamano hili la STICE na hata wale watakaoshindwa kuhudhuria kwasababu tofauti tofauti wafuatulie kongamano hili kwenye luninga kwasababu litakuwa mubashara,
โUshiriki wenu ni muhimu sana katika kuleta mawazo na mikakati mipya, kuimarisha utafiti na ubunifu, na kuhakikisha kuwa matokeo ya utafiti na ubunifu yanajibu mahitaji na kutatua changamoto za maendeleo ya kiuchumi na kijamii,โamesema Prof.Mkenda.
ย
The post ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐ appeared first on Mzalendo.