Nini kinatokea ikiwa mgombea atatangaza ushindi mapema? – DW – 06.11.2024

Wakati Kamala Harris anaongoza kwa asilimia 1-2 katika kura za umma, mfumo wa kura za wajumbe wa majimbo unaojulikana kama Electoral Colleage, unawapa faida Warepublikani, hasa Donald Trump, na majimbo saba muhimu yanatarajiwa kuamua matokeo. Hali ya ushindani mkali, kanuni tofauti za kupigia kura, na uwezekano kwamba mshindi halisi anaweza asiwe wazi kwa siku kadhaa, baadhi ya waangalizi wana wasiwasi kwamba Trump  anaweza kwa mara nyingine kujitangazia ushindi wa mapema.

Tangu uchaguzi uliopita, Trump amekuwa akilaumu maafisa wa uchaguzi kwa udanganyifu na kudhoofisha mtazamo wa umma kuhusu uhalali wa chaguzi za Marekani. Kauli hizi zinaweza kuhatarisha mchakato wa uchaguzi, hivyo ni muhimu kutathmini hatari zinazohusiana na changamoto hizi na kubaini hatua zinazochukuliwa ili kuimarisha uaminifu wa uchaguzi na kuhakikisha matokeo halali, bila kujali mitazamo ya kisiasa.

Soma pia: Marekani yaamua: Chaguo ni kati ya Trump na Harris

Baada ya kituo cha Fox News kutangaza kuwa Joe Biden ameshinda Arizona katika uchaguzi wa 2020, Donald Trump alikosoa vikali vyombo vya habari kwa kutangaza matokeo, akidai kuwa uchaguzi ulikuwa umepangwa na umeporwa. Hali hii ilisababisha ghasia zilizopelekea uvamiszi wa majengo ya bunge ya Capitol Hill mnamo Januari 6, 2021, ambapo wafuasi wake walijaribu kuvuruga uthibitishaji wa ushindi wa Biden.

Marekani | Hatua za kiusalama kuzunguka Ikulu ya White House
Mwanachama wa Kikosi cha Ulinzi wa Viongozi Marekani akifunga lango la usalama kando ya Mtaa wa Pennsylvania karibu na Ikulu ya White House siku moja kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani mjini Washington, Marekani, Novemba 4, 2024.Picha: Nathan Howard/REUTERS

Trump na wafuasi wake waliwasilisha zaidi ya mashtaka 60 kujaribu kupinga matokeo, lakini ni moja pekee lililoonekana kuwa na mashiko, na wataalamu walikubali kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Wataalamu wa sheria wanasema mfumo wa uchaguzi ulionyesha uhimili na utatoa changamoto kubwa kwa Trump ikiwa atajaribu kutangaza ushindi wa awali tena.

Nini kitatokea iwapo Trump atatangaza ushindi wa mapema?

Ingawa uchunguzi wa maoni unaonesha Trump na Harris wanakaribiana sana, kosa la kawaida la uchunguzi wa maoni linaweza kumaanisha kuwa mgombea yeyote anaweza pia kushinda kwa kishindo. Ikiwa Trump atadai ushindi wa awali huku majimbo muhimu yakiwa bado hayajakamilisha hesabu, vyombo vya habari vitabaki na jukumu muhimu katika kutangaza matokeo.

Uamuzi wa Fox News kutangaza ushindi wa Biden jimboni Arizona mnamo 2020 unaonyesha kwamba upendeleo wa jadi unawekwa kando katika kuhakikisha usahihi wa matokeo. Wademokrati wamejiandaa kupinga tangazo la ushindi wa mapema, huku Kamala Harris akisema watajibu ikiwa Trump atajaribu kudanganya umma.

Soma pia: Uchaguzi Marekani: Washington yasalia tulivu kabla ya kivumbi

Wapiga kura wengi wanatarajia Trump kukataa matokeo yasiyokuwa katika upande wake; uchunguzi wa CNN unaonyesha kuwa ni asilimia 30 tu wanaamini atakubali kushindwa. Kila jimbo lina kanuni zake kuhusu hesabu za kura na uthibitisho wa washindi, na mchakato huu utaendelea hadi majimbo yote na Washington D.C. yatakapotoa matokeo yao.

Richard Pildes anasema, “mgombea anaweza kutangaza ushindi kadri anavyotaka, lakini kama jumla za kura haziko katika upande wake, atashindwa,”  na kuongeza kuwa matokeo haya yanaweza kuwa ya kitamaduni au kisiasa.

Harris kuchuana vikali na Trump. Nani kuibuka mshindi leo?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Je, mgombea anaweza kupinga uchaguzi? 

Hakuna chochote kinachomzuia mgombea yeyote kupinga uchaguzi. Kama ilivyokuwa mnamo 2020, wakati Trump na wafuasi wake walipowasilisha pingamizi nyingi za kisheria kuhusu mchakato wa uchaguzi, mgombea lazima awasilishe malalamiko yake katika mahakama.

Kamati ya Kitaifa ya chama cha Republican inaripotiwa kuwa imewasilisha mapingamizi 130 za kisheria tayari, hasa katika majimbo yanayobadilika. Wademokrati pia wameweka timu za kisheria nchini kote kukabiliana na madai ya Warepublikani kuhusu udanganyifu wa kura.

“Pingamizi hizo zitawasilishwa mahakamani, na bila shaka natarajia kuona baadhi yake kulingana na jinsi uchaguzi unavyokaribia,” alisema Pildes.

Soma pia: Uchaguzi Marekani: Harris na Trump katika kampeni za mwisho

“Hakuna kosa lolote katika hilo; tunataka mizozo itatuliwe sheria, tunataka itatuliwe katika mahakama, siyo sehemu nyingine, hivyo kadri kunapokuwa na msingi mzuri wa kisheria na wa kifahamu wa kuibua masuala fulani baada ya uchaguzi katika mahakama, hiyo ni sawa. Hiyo ni haki ambayo wagombea wanayo,” aliongeza.

Ni akina nani wengine hupigiwa kura Marekani?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Kupanga mashambulizi itakuwa vigumu zaidi 2024 

Je, kuna uwezekano kwamba tukio kama lile la 2021, ambapo waandamanaji walivamia Jengo la Capitol, litajitokeza tena?

Tsai haamini hivyo. Kwanza, Biden atabaki kuwa rais hadi mrithi wake atakapoapishwa. Tsai anasema Trump hayuko Ikulu “hivyo hawezi kukataa kuondoka.”

“Ni vigumu sana kuhamasisha ghasia wakati huwezi kutegemea watu kutoka Ofisi ya Rais.” Lakini, hiyo haimaanishi kuwa mitazamo iliyopo kuhusu uchaguzi usio wa haki haiwezi kuzua machafuko, Tsai alieleza, akiongeza kuwa “ni vigumu kufikiria kwamba Wizara ya Sheria ya [utawala wa] Biden hawako tayari.”

Tsai anabaini kuwa timu ya Biden imeyaarifu majimbo fulani “kwamba wanataka kuwa na uwepo katika maeneo fulani ndani ya majimbo hayo kwa sababu ya mambo yaliyotokea hapo awali au kwa sababu ya vitu fulani walivyogundua, hasa kupitia FBI.”

“Kama kweli kuna hatari yoyote ya shughuli za juu za uasi wa aina hiyo, nadhani tayari tuna rasilimali za kutosha kuweza kuingilia kati,” alisema Tsai.

Related Posts