PROF. MWAKALILA AZUNGUMZA NA WANAFUNZI WAPYA WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE ASISITIZA UADILIFU NA UZALENDO

Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amewataka wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo 2024/25 wa Chuo hicho kuwa Wadilifu,Waaminifu na Wazalendo kwa Chuo na Taifa kwa ujumla.

 
Prof. Mwakalila amesema hayo leo wakati wa kikao cha pamoja Kati ya Wafanyakazi na Wanafunzi hao wapya kikao ambacho kinefanyika katika Jengo la Utamaduni Chuoni hapo.

Katika kikao hicho Prof. Mwakalila amewataka Wanafunzi kuzingatia kanuni, miongozo na taratibu za Chuo ikiwa ni pamoja na kujiepusha na makundi ya uchochezi na badala yake wabakie kwenye malengo yaliyowaleta Chuoni.

Mkuu huyo wa Chuo amewakumbusha Wanafunzi suala la kuheshimiana wao kwa wao, kuheshimu viongozi na Wafanyakazi na kuheshinu Mamlaka zote.

Mkuu wa Chuo pia amewataka wanafunzi kuitumia vizuri Serikali ya Wanafunzi katika kutatua changamoto mbalimbali katika kipindi chao chote watakachokuwa chuoni hapa Prof. Shadrack Mwakalila amesema dira ya Chuo ni kuwa kituo cha utoaji wa maarifa bora, hivyo majukumu ya Chuo hiki ni majukumu Kama yalivyo kwenye Vyuo Vikuu vingine hapa nchini.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Taaluma,Utafiti, na Ushauri wa kitaalamu Prof. Richard Kangarawe amewataka Wanafunzi kukamilisha usajili ili waweze kupata huduma wanazostahili kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuzingatia Sheria za mitihani ili wahitimu kulingana na programu husika na kwa wakati unaotakiwa.

Naye Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Utawala, Fedha na Mipango Dkt. Evaristo Haule amewaeleza wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza kuwa wamefanya chaguo sahihi kuja kusoma katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, na kuwa watapata Elimu bora inayozingatia Maadili.

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 6.11.2024

Related Posts