KASHWASA  YAFANYA KAZI SAA 24 KUREJESHA MAJI KISHAPU

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanya (KASHWASA) imefanya kazi saa 24 kwa wataalam wake kurejesha huduma ya maji kwa wakazi wa Kishapu.

Kazi hiyo imehusu kuweka viungo muhimu vya chuma katika bomba kuu linalotegemewa katika huduma ya maji.

Hivi sasa Kishapu inapata huduma ya uhakika ya majisafi, salama na yenye kutosheleza tangu tarehe 4 Novemba 2024. Ufuatiliaji wa huduma ya maji kwa wananchi unafanyika kwa saa 24 katika bomba kuu la kusafirisha maji.

Related Posts