Mji huo mkuu ulio na idadi ya zaidi ya watu milioni moja, ulikuwa mtulivu bila heka heka zozote asubuhi ya Alhamis huku maduka, benki, shule na vyuo vikuu vikifungwa. Baadhi ya waandamanaji walikusanyika kuanzia majira ya saa moja asubuhi katika moja ya mitaa mikuu kabla ya kuamriwa na wanajeshi kurudi nyumbani.
Soma: Mamlaka Msumbiji zatishia kutumia jeshi kudhibiti maandamano
Mgombea wa upinzani, Venancio Mondlane, ambaye anaamini kwamba alishinda uchaguzi huo, alikuwa ameitisha maandamano makubwa nchini humo siku ya Alhamis. Katika mahojiano na shirika la habari la AFP, kiongozi wa upinzani ambaye hajulikani yuko wapi amesema kuwa hatoshiriki maandamano kutokana na hofu ya usalama wake.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kuwa karibu watu 18 wameuwawa katika machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi huo. Lakini shirika lisilo la kiserikali nchini humo la Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu, CDD, limesema kuwa idadi ya waliofariki ni watu 24.
Afisa mmoja wa polisi pia aliuawa katika maandamano ya mwishoni mwa juma, kwa mujibu wa waziri wa ulinzi Cristovao Chume kama alivyozungumza na waandishi wa habari Jumanne, akionya kwamba jeshi huenda likaingilia kati ili “kulinda maslahi ya taifa”. “Kuna dhamira ya kubadilisha mamlaka iliyoanzishwa kidemokrasia”, ameongeza waziri huyo katikati mwa wasiwasi kwamba rais anayeondoka madarakani Filipe Nyusi anaweza kutangaza hali ya tahadhari. Nyusi anatarajiwa kuondoka mamlakani mapema mwakani mwishoni mwa muhula wake wa pili. Wasiwasi watanda Msumbiji kabla ya maandamano ya upinzani
Taifa hilo la kusini mwa Afrika limekumbwa na ghasia tangu uchaguzi wa Oktoba 9 ambao umempatia ushindi mgombea wa chama tawala cha Frelimo, kilichokuwepo madarakani kwa karibu miaka 50. Mgombea wa Frelimo Daniel Chapo alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 71 ya kura, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi huku mpinzani wake Venancio Mondlane akiibuka nafasi ya pili na 20%.
Shirika la Human Rights Watch HRW limesema mamlaka nchini humo zimezuia upatikanaji wa huduma za intaneti kote nchini katika kile kinachoonekana kama juhudi za “kubinya maandamano ya amani na ukosoaji wa umma dhidi ya serikali.”Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Msumbuji yageuka vurugu
Mkurugenzi wa uhamasishaji Afrika wa HRW Allan Ngari amesema “uzuiaji wa intaneti unawanyima uwezo watu wa kupokea na kuzitumia taarifa, kukusanyika kwa amani na kuelekea maoni yao ya kisiasa wakati wa mzozo”.Chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji chaomba kura kuhesabiwa upya
Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk alisema siku ya Jumatano kwamba “ana wasiwasi mkubwa na ripoti za vurugu kote nchini.” Ametaka polisi kujizuia kutumia nguvu kupita kiasi na kuhakikisha wanadhibiti maandamano kwa kuzingatia haki za binadamu.