RAIS DKT.MWINYI KUZINDUA OFISI NA MAABARA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA ZANZIBAR

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wahabari leo Novemba 7,2024 jijini Dodoma kuhusu uzinduzi wa Ofisi na maabara za Tume  ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) zilizojengwa eneo la DungaZuze Zanzibar 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga,akizungumza na waandishi wahabari kuhusu uzinduzi wa Ofisi na maabara za Tume  ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) zilizojengwa eneo la DungaZuze Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akizungumza na waandishi wahabari kuhusu uzinduzi wa Ofisi na maabara za Tume  ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) zilizojengwa eneo la DungaZuze Zanzibar.

Mwenyekiti wa Bodi ya TAEC Prof Joseph Msambichaka,akielezea   Taasisi hiyo inaendelea na juhudi za kutoa Elimu kwa Umma juu ya Taasisi hiyo na faida za teknolojia kuhusu uzinduzi wa Ofisi na maabara za Tume  ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) zilizojengwa eneo la DungaZuze Zanzibar.

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof. Najat Kassim Mohammed,,akizungumza  kuhusu uzinduzi wa Ofisi na maabara za Tume  ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) zilizojengwa eneo la DungaZuze Zanzibar.

Na.Alex Sonna-DODOMA

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi anatarajia kuzindua ofisi na maabara za Tume  ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) zilizojengwa eneo la DungaZuze Zanzibar  ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa serikali wa kusogeza huduma kwa wananchi.

Hayo yameelezwa leo Novemba 7,2024 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi huo unaotarajia kufanyika Novemba 11,mwaka huu.

Prof. Mkenda amesema uwepo wa Maabara Mpya ya Nguvu za Atomu upande wa Zanzibar ni hatua muhimu katika kuhakikisha matumizi ya teknolojia ya nyuklia yanakua na kuleta tija inayokusudiwa.

“Huu ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo Tume ilielekezwa kuhakikisha kuwa inaendelea kuimarisha huduma, tafiti na ubunifu unaolenga kuongeza wigo wa matumizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia katika sekta mbalimbali nchini na kuhamasisha matumizi salama ya nyuklia karibu na wananchi wa Zanzibar,”amesema Prof.Mkenda

Aidha ameeleza  kuwa teknolojia hiyo inatumika kuchunguza na kutibu ugonjwa wa saratani, kuboresha mbegu za mazao hasa yale ambayo yanaugumu kustawi na yanatoa mazao kidogo, kuua vimelea vinavyosabisha chakula kuharibika kudhibiti kuzaliana kwa wadudu wanaoeneza magonjwa kama vile mbung’o.

Prof.Mkenda amesema wizara yake kwa kushirikiana na Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania wamejenga ofisi na maabara hizo za nyuklia katika kanda nne ambazo ni Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Kati (Dodoma), Kanda ya Ziwa (Mwanza) na hivi karibuni watazindua Ofisi ya Zanzibar kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Prof.Mkenda Serikali kupitia skolashipu ya ‘Samia Extended’ inalenga kusomesha vijana watano wa Kitanzania nje ya nchi katika ngazi ya Umahiri kwenye masuala ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia.

“Kutokana na uhaba wa wataalamu wa Sayansi ya nguvu za Nyuklia, kupitia ufadhili wa Samia Scholarship Extended  Watanzania watano wamepata Ufadhili huo na wanaenda kusomea taaluma hiyo katika Nchi za Austria, Afrika Kusini, Uingereza, Canada na Italia katika Vyuo Vikuu Bora vinavyotoa mafunzo ya Teknolojia ya Nuklia.”amesema Prof.Mkenda

Hata hivyo Prof,Mkenda ametoa  wito kwa vijana wa kitanzania kusomea eneo hilo ili wapate fursa ya kuendelezwa na serikali kupata ujuzi stahiki.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga amesema Teknolojia ya Nyuklia ina manufaa mengi katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya , Kilimo nakusisitiza kuwa Wizara inaendelea kuimarisha Uthibiti wa matumizi yake na kuhimiza matumizi sahihi katika maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TAEC Prof Joseph Msambichaka  amesema Taasisi hiyo inaendelea na juhudi za kutoa Elimu kwa Umma juu ya Taasisi hiyo na faida za Teknolojia.

Related Posts