Yanga yaitisha kikao cha dharura usiku, Gamondi kikaangoni

Saa chache baada ya Yanga kupoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Tabora United, kimeitishwa kikao kizito cha Kamati ya Utendaji cha pili kwa siku kikimjadili kocha wa timu hiyo Miguel Gamondi.

Mapema leo asubuhi Yanga ilikuwa na kikao cha Kamati ya Utendaji lakini kimelazimika kurudiwa tena usiku kwa dharura kufuatia matokeo ya timu hiyo baada ya kuchapwa dhidi ya Tabora United.

Mwanaspoti limethibitishiwa kuwa kikao hicho kinaendelea muda huu kwenye ofisi za Rais wa Yanga Mhandisi Hersi Said zilizopo Jengo la Salamanda.

Related Posts