Yanga Oktoba freshi, balaa limeanzia huku

YANGA imeuanza Novemba na mguu mbaya baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo tena ikiwa nyumbani, ikianza kwa kuchapwa 1-0 na Azam kabkla ya juzi kufumuliwa na Tabora United kwa mabao 3-1.

Kipigo cha Tabora ni cha kwanza kikubwa kwa Yanga ndani ya miaka minne katika Ligi Kuu, kwani mara ya mwisho ilifungwa 3-0 na Kagera Sugar jijini Dar es Salaam katika mechi iliyopigwa Janua15, 2020, pia ni cha kwanza kwa vijana wa Jangwani mbele ya Tabora tangu timu hiyo ilipopnda daraja msimu uliopita.

Hata hivyo, pamoja na machungu hayo ya kuanza Novemba na mguu mbaya, lakini watetezi hao wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho na waliopo makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ilikuwa na mambo matamu ndani ya mwezi uliopita wa Oktoba, licha ya kocha wake, Miguel Gamondi kushindwa kupewa tuzo ya Kocha Bora.

Hapa chini ni rekodi tamu za Yanga ndani ya Oktoba ambazo ziliifanya timu hiyo kufunika zaidi ya klabu nyingine 15 zinazoshiriki ligi hiyo iliyopo raundi ya 11 na kwa sasa imesimama kwa wiki mbili ili kupisha wiki ya kalenda ya michuano ya kimataifa kwa timu za taifa.

Picha Pict
Picha Pict

Yanga haikupoteza mchezo wowote ndani ya Oktoba ikishinda mechi zote tano za Ligi Kuu Bara ilizocheza ikiunza mwezi huo kwa kuichapa Pamba Jiji 4-0 (Oktoba 3), kisha ikainyuka Simba kwa bao 1-0 (Oktoba 19).

Baada ya mechi hizo wakafuata JKT Tanzania iliyolala 2-0 (Oktoba 22), halafu wakafuatia Wagosi w Kaya, Coastal Union waliokufa 1-0 (Oktoba 26) nakufunga mwezi huo kwa kuicharaza Singida Black Stars kwa baoa 1-0 (Oktoba 30).

Picha01
Picha01

Ndani ya ushindi wa mechgi hizo hakuna mechi ambayo Yanga iliwapa raha kama kuwachapa watani wao wa jadi Simba, ushindi ambao unaweza kupoza maumivu yoyote watakayopata kutokana na ushindani na rekodi ya mchezo huo mkubwa kwa klabu hizo kongwe.

Itakumbukwa ushindi huo dhidi ya Simba, Yanga iliweka rekodi ya kuendelea kuwanyanyasa watani wao kwa mchezo wa tatu mfululizo wakiwachapa wekundu hao.

Picha02
Picha02

Oktoba hiyohiyo Yanga ikaitumia kurudi juu ya msimamo wa ligi ikipanda hapo kwa mara ya kwanza tangu msimu uanze ikiishusha Singida Black Stars iliyokaa hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Singida ndio timu iliyokuwa na mafanikio nyuma ya Yanga ndani ya Oktoba ambayo ilicheza mechi nne ikishinda tatu na kupoteza mchezo mmoja walipofungwa na mabingwa hao watetezi.

Ubabe wa Yanga zaidi ni kwamba ndani ya mwezi Oktoba ikafunga jumla ya mabao tisa ikizifunga timu tano tofauti huku hakuna timu iliyofanikiwa kufunga bao lolote kwenye nyavu za timu hiyo, mabingwa hao wakionyesha ubabe wa ukuta wao.

Hersi
Hersi

Nje ya Uwanja Yanga ikapokea taarifa njema za heshima kufuatia Rais wao injinia Hersi Said kujishindia tuzo ya mwanamichezo mwenye mchango kwenye maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika.

Sherehe ya ugawaji wa tuzo hizo zilifanyika jijini Paris, Ufaransa,Oktoba 21,2024 rais huyo akipokelewa tuzo yake na Balozi wa Tanzania nchini humo Ali Jabir Mwadini.

Licha ya kiwangio kilichoonyeshwa na Yanga ndani ya Oktoba na kufikiriwa huenda kocha Miguel Gamondi anangeibuka kocha bora wa mwezi, tuzo hiyo imeeenda kwa Rachid Taoussi wa Azam aliyeshinda mechi tatu ndani ya mwezi huo, huku Diarra aliyekuwa kinara wa clean Sheet akitoka patupu baada ya Kamati ya tuzo ya ya Bodi ya Ligi kumpa Marouf Tchakei wa Singida BS aliyefunga mabao matatu katika mechi hiyo za timu yake, ambayo ilishinda tatu na kupoteza moja mbele ya Yanga.

Tchakei alifunga mabao mawili ya kawaida na jingine la penalti na kuiwezesha timu yake kukusanya pointi tisa katika mechi hizo tatu, huku Taoussi katika mechi tatu alishinda zote tatu na kukusanya pointi tisa, mabao saba na kufungwa moja, akiwa yupo nyuma ya Gamondi aliyekusanya pointi 15 na mabao tisa bila kuruhusu bao lolote kabla ya mambo kumchachia Novemba akipoteza mechi mbili mfululizo na kuruhusu mabao manne na funga moja tu.

Nini kitakachofuata baada ya ligi kurudi Novemba, ni suala la kusubiri kuona, ila kwa Oktoba bila kuuma maneno, Yanga ndio walikuwa baba lao!

Related Posts