KATIBU MKUU UWT APOKEA TARAKILISHI 34

📍 8 Novemba, 2024~Dodoma

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), *Ndg. Suzan Kunambi (MNEC)* amepokea jumla ya tarakilishi (computer) 34 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum, *Mhe. Stella Ikupa*.

Tarakilishi hizo zitasambazwa na kukabidhiwa katika ofisi za Makao Makuu ya UWT pamoja na Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuongeza ufanisi, ubunifu na utendaji bora wa UWT katika Mikoa yote nchini.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, Kunambi ameshukuru sana kwa msaada huo uliotolewa na amewaalika wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono Jumuiya hii ili kuchochea ustawi wake.

#uwtimara
#jeshiladktsamianadktmwinyi

Related Posts