Maseke matumaini kibao makubwa KMC

KIPA wa KMC, Wilbol Maseke amesema licha ya msimu kuanza msimu ‘akichomeshwa’ mahindi benchi, bado anaamini ana nafasi kubwa ya kutumika kikosini kwani muda upo, ila kazi aliyonayo ni kuhakikisha anapambana na kuzingatia nidhamu kumshawishi kocha kumpa nafasi ya kucheza kupitia uwanja wa mazoezi.

Kocha huyo wa zamani wa Azam FC, alisema anafahamu ndani ya KMC kwa sasa kuna ushindani wa namba kutokana na kuongezwa watu katika nafasi ya kipa akiwamo Mrundi Fabien Mutombora, na kama mchezaji anafurahia kwani inamfanya asilale ila kupambana kwa kuongeza bidii katika mazoezi kila uchao.

“Ukitazama makipa wameimarika na kupunguza makosa mengi, ndio maana mabao yamepungua na washambuliaji wanapata shida kufunga, ingawa wanapambana kwa kadri wanavyoweza. Nimeona washambuliaji jinsi  wanapoteza nafasi nyingi  za kufunga, hilo linatokana na presha kubwa kutoka kwa mabeki, hilo ni jambo zuri linaonyesha jinsi ligi inavyopiga hatua.

Mbali na hilo, pia Maseke aliizungumzia pia hali ya Ligi Kuu ilipofikia analitaja bao bora kwake kwa sasa ni lile lililofungwa na nyota wa Coastal Union, Mkenya Abdallah Hassan dhidi ya Simba alipoisawazishia timu hiyo katika sare ya 2-2 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa KMC Complex.

“Sidhani hata kama kipa wa Simba, Moussa Camara kama alitarajia kukutana na ugeni wa shuti kama lile golini kwake. Kwa kweli namsifu mpigaji, kwani alijiongeza na kumsoma kipa alipo ni kama hakuwa na utayari wa kuona mpira unaelekezwa kwake na akamtungua, wangu ni bao bora hadi sasa,” alisema Maseke mwenye clean sheet moja.

Related Posts