Dar es Salaam. Miongoni mwa habari zilizostua leo ni kifo cha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrance Mafuru ambaye amefariki dunia leo, akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Apollo nchini India.
Mafuru aliyekuwa mtaalamu wa fedha na uchumi maarufu hapa nchini, amehudumu katika taasisi kubwa tofauti kwa miongo zaidi ya miwili. Hapa tunaangazia safari yake ya kikazi hadi umauti ulipomkuta.
Baada ya kumaliza Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM), Mafuru alipata kazi Benki ya Standard Chartered Tanzania (1998 -2000) akifanya kazi ya kusimamia biashara na fedha za kimataifa.
Baadaye alihudumu kama ofisa wa wateja wakubwa kisha meneja wa miamala ya kibenki, maendeleo ya biashara na hadi kuwa mkuu wa mauzo na viwango vya kubadilishia fedha za kigeni.
Mwaka 2007 hadi 2010 akateuliwa kuwa rais wa Umoja wa soko la fedha Tanzania wakati huo akiwa mhazini wa benki ya NBC kisha akawa Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) kuanzia mwaka 2010 hadi 2012. Wakati huo alikuwa ofisa mtendaji mkuu wa NBC Tanzania.
Mwaka 2013 wakati wa utawala wa awamu ya nne, aliingia serikalini na kuanza kazi kama kiongozi wa ukusanyaji wa rasilimali chini ya mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na baadaye akawa Mkurugenzi wa idara ya makusanyo ya ndani na sekta za uchumi chini ya Ofisi ya Rais (PDB).
Mwaka 2013 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Kituo cha Taifa cha uwekezaji na mwaka mmoja baadaye akawa mjumbe huru wa bodi ya benki ya CRDB hadi mwaka 2016.
Mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Msajili wa Hazina nafasi ambayo alidumu kwa miaka miwili kabla ya kuondolewa na Rais John Magufuli katika uamuzi ulioibua gumzo hapa nchini.
Baada ya kuondolewa serikalini mwaka 2017, Mafuru alifungua kampuni binafsi iitwayo Benkable ambayo inatoa ushauri wa masuala ya kifedha.
Baada ya Rais Samia Suluhu kushika uongozi wa nchi kufuatia kifo cha hayati John Magufuli, Mafuru alirudi tena serikalini na kazi yake ya kwanza alihudumu kama Kamishna wa uchambuzi wa sera wa Wizara ya Fedha.
Mwaka mmoja baadaye (2022) alipandishwa cheo na kuwa Naibu Katibu Mkuu anayesimamia sera za uchumi na Julai 2023 aliteuliwa kuwa Kamishna wa Mipango.
Mpaka anafariki, alikuwa mjumbe wa bodi ya Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) na bodi ya wadhamini wa Wakifu wa Benjamin Mkapa.
Huyu ndiye Mafuru, mtaalamu bingwa wa fedha na uchumi
- Lawrence Mafuru alizaliwa mwaka 1972 na baadaye, akasoma Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kuhitimu mwaka 199
- Mafuru aliyekuwa mtaalamu wa fedha na uchumi maarufu hapa nchini, amehudumu katika taasisi kubwa tofauti kwa miongo zaidi ya miwili. Hapa tunaangazia wasifi wake kikazi hadi umauti ulipomkuta.
- Baada ya kumaliza Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM), Mafuru alipata kazi Benki ya Standard Chartered Tanzania (1998 -2000) akifanya kazi ya kusimamia biashara na fedha za kimataifa.
- Baadaye alihudumu kama ofisa wa wateja wakubwa kisha meneja wa miamala ya kibenki, maendeleo ya biashara na hadi kuwa mkuu wa mauzo na viwango vya kubadilishia fedha za kigeni.
- Mwaka 2007 hadi 2010 akateuliwa kuwa rais wa Umoja wa soko la fedha Tanzania wakati huo akiwa mhazini wa benki ya NBC kisha akawa Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) kuanzia mwaka 2010 hadi 2012. Wakati huo alikuwa ofisa mtendaji mkuu wa NBC Tanzania.
- Mwaka 2013 wakati wa utawala wa awamu ya nne, aliingia serikalini na kuanza kazi kama kiongozi wa ukusanyaji wa rasilimali chini ya mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na baadaye akawa Mkurugenzi wa idara ya makusanyo ya ndani na sekta za uchumi chini ya Ofisi ya Rais (PDB).
- Mwaka 2013 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Kituo cha Taifa cha uwekezaji na mwaka mmoja baadaye akawa mjumbe huru wa bodi ya benki ya CRDB hadi mwaka 2016.
- Mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Msajili wa Hazina nafasi ambayo alidumu kwa miaka miwili kabla ya kuondolewa na Rais John Magufuli katika uamuzi ulioibua gumzo hapa nchini.
- Baada ya kuondolewa serikalini mwaka 2017, Mafuru alifungua kampuni binafsi iitwayo Benkable ambayo inatoa ushauri wa masuala ya kifedha.
- Baada ya Rais Samia Suluhu kushika uongozi wa nchi kufuatia kifo cha hayati John Magufuli, Mafuru alirudi tena serikalini na kazi yake ya kwanza alihudumu kama Kamishna wa uchambuzi wa sera wa Wizara ya Fedha.
- Mwaka mmoja baadaye (2022) alipandishwa cheo na kuwa Naibu Katibu Mkuu anayesimamia sera za uchumi na Julai 2023 aliteuliwa kuwa Kamishna wa Mipango.
- Mpaka anafariki, alikuwa mjumbe wa bodi ya Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) na bodi ya wadhamini wa Wakifu wa Benjamin Mkapa.