GF Vehicles Assemblers yashinda tuzo za Rais kwa uunganishaji magari nchini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kiwanda cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani kimeibuka mshindi wa kwanza kwa makampuni ya Kati nchini wakati wa utoaji wa tuzo za Rais kwa wazalishaji bora (President’s Manufacturer of the year Awards – PMAYA) zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho , Ezra Mereng amesema anawapongeza wafanyakazi wake kwa umoja wao ndio chachu ya mafanikio ya wao kukidhi ubora katika uzalishaji wa magari bila wao wasingeweza kufanikiwa katika ushindi wa tuzo hiyo ambayo ni ya pili kwa kampuni ya GFA.

Nae Mkurugenzi wa Masoko na Mawasilianao wa Kampuni hiyo, Salman Karmali amesema wao kama kampuni wanashukuru tuzo hiyo ni dalili nzuri kwani kiwanda hicho cha kuunganisha magari nchini ndio kiwanda cha kwanza  hapa Tanzania kunganisha magari makubwa  pia tunajivunia  kuwa waongoza njia katika sekta ya Usafirishaji.

Pia Karmali amesema GFA ni kiwanda kikubwa kilichopo kibaha mkoani Pwani na kutokana na mafanikio wanaingia katika hatua ya pili ya upanuzi na uzalishaji ambapo wanatarajia katika upanuzi huu  awamu ya pili kutengeneza magari 10(trucks) kwa siku kutoka magari 4 ambayo kwa itaunganisha magari makubwa na madogo.

Ameeleza kuwa mkakati wao.ni kulifikia soko la ndani na nje ili kuliiingizia Taifa fedha za kigeni kwa kuuza magari katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika watumie bidhaa kutoka Tanzania jambo ambalo hapo zamani halikuzoeleka miongoni mwa magari hayo ni FAW, HONG YAN na FOLAND

Tunaipongeza serikali kuweka mazingira mazuri hasa sheria ya ‘Local Content’ kuwawezesha Watanzania kufanya kazi mbalimbali na kutoa huduma migodini na miradi ya serikali hali iliyokuza vipato vya Watanzania wengi na kumudu kununua magari kutoka kiwandani kwetu alimaliza Karmali.

Related Posts