𝐂𝐂𝐌 𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐌𝐆𝐔𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐆𝐔𝐔 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐁𝐀𝐋𝐎𝐙𝐈 𝐊𝐔𝐄𝐋𝐄𝐊𝐄𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔 𝐖𝐀 𝐒𝐄𝐑𝐈𝐊𝐀𝐋𝐈 𝐙𝐀 𝐌𝐈𝐓𝐀𝐀

Uongozi wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini chini ya Mwenyekiti Charles Mamba umeendelea na mikutano ya mfufulizo na mabalozi wote 2000 wa Jimbo la Dodoma Mjini katika kujiweka sawa kuelekea katika uchaguzi wa serikali wa mitaa ambapo leo kikao kimefanyika cha Mabalozi kutoka Kata ya Makutupora,Chihanga,Ipala,Chahwa,Hombolo Makulu na Hombolo Bwawani.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CCM wilaya *Ndg. Charles Mamba amewapongeza Mabalozi kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya na kuwataka kuhimiza wanaCCM kushiriki kwa wingi katika Uchaguzi huo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewapongeza mabalozi kwa kazi nzuri waliyofanya ya uhamasishaji wananchi kujiandikisha katika daftari la wakazi na kuwataka kufanya kazi nzuri kuwahamasisha wananchi wengi zaidi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo wa serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27.11.2024

Mkutano huo ulienda sambamba na ugawaji wa vitendea kazi kwa mabalozi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.





Related Posts