Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI chini ya mwenyekiti wake Justin Nyamoga leo imezielekeza Halmashauri zote nchi kuiga mbinu na njia bora zilizotumika katika utekelezaji wa Shirika la
Maendeleo la Jiji la Dar es salaam (DDC) katika eneo la Karikoo kupitia ubia Kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP).
Mhe. Nyamoga ametoa maelekezo hayo katika majumuisho mara baada ya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia PPP katika Mkoa wa Dar es salaam.
Kamati hiyo imetembelea na kukagua mradi huu wa soko la maduka yajulikanayo kama DDC Kariakoo unaojengwa na mwekezaji mzawa kupita PPP na Barabara ya magomeni mapipa kupitia Mradi wa DMDP awamu ya kwanza kwa kiwango cha lami kwa lengo la kupunguza foleni.
“Halmashauri zenye fursa” za kiuchumi zinafaa kujifunza kutoka kwa Mkoa wa Dar es salaam namna bora ya uratibu na uendeshaji wa miradi ya PPP”
Aidha Mhe. Nyamoga ameielekeza TARURA mkoani humo kuendelea kuzingatia usafi na kutunza miradi hiyo ya Barabara ili itumike kwa muda mrefu zaidi.
Akionge kwa niaba ya Naibu Waziri, Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka OR – TAMISMI Bw. John Mihayo Cheyo amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI imepokea maelekezo yote yaliotolewa na kamati na kuahidi kuyasimia vyema katika utekelezaji.