DKT. BITEKO AIPONGEZA DODOMA JIJI  KUVUKA LENGO UANDIKISHAJI WAPIGA KURA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Dodoma Mjini uliyolenga kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mwaka 2020 hadi 2024  uliofanyika leo Novemba 10,2024 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Dodoma Mjini uliyolenga kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mwaka 2020 hadi 2024  uliofanyika leo Novemba 10,2024 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Dodoma Mjini uliyolenga kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mwaka 2020 hadi 2024  uliofanyika leo Novemba 10,2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde,akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Mwaka 2020 hadi 2024, katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Dodoma Mjini uliofanyika leo Novemba 10,2024 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel,akizungumza ,wakati wa  Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Dodoma Mjini uliyolenga kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mwaka 2020 hadi 2024  uliofanyika leo Novemba 10,2024 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba,,akizungumza ,wakati wa  Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Dodoma Mjini uliyolenga kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mwaka 2020 hadi 2024  uliofanyika leo Novemba 10,2024 jijini Dodoma.

Wanachama wa CCM Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,(hayupo pichani) wakati wa  Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Dodoma Mjini uliyolenga kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mwaka 2020 hadi 2024  uliofanyika leo Novemba 10,2024 jijini Dodoma.

…….

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuandikisha idadi kubwa ya wananchi katika daftari la wapiga kura ikiwa ni maandalizi ya Uchanguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo leo Novemba 10, 2024 wakati akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Dodoma Mjini uliyolenga kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mwaka 2020 hadi 2024.

“Kipekee kabisa niwapongeze Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kufanya vizuri zaidi kuliko Halmashauri yoyote nchini kwa uandikishaji uliovuka lengo mpaka kufikia asilimia 128 ya lengo la uandikishaji. Hii ni kuthibitisha kwamba Mkoa wa Dodoma mmejipanga vizuri sana kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao,” amesema Dkt. Biteko.

Pia, Dkt. Biteko ametoa pongezi kwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo imeleta manufaa makubwa katika ustawi wa jiji la Dodoma.

“Ninampongeza sana Mbunge wenu Mhe. Anthony Peter Mavunde kwa tukio la leo la uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2024 pamoja na kukabidhi vitendea kazi kwa viongozi kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Nimefurahishwa kwa namna ambavyo zimefanyika kazi kubwa za kugusa maisha ya watu na hasa watu wenye kipato cha chini na kuwa karibu na wananchi,” amesema Dkt. Biteko.

Amesisitiza “Nataka niwaambie watu wa Dodoma Mhe. Mavunde ana sifa nyingi nataka nitaje chache, Mbunge wenu anajua ubunge alionao si wake ni wa CCM na wanachama wake hivyo wakati wote amekuwa mtu anayeshughulika na shida za watu, mtu anayefanya kazi na anastahili kuambiwa akiwa hai yeye anafanana na watu walipewa talanta na yeye  anafanana na aliyepewa talanta tano,”

Aidha, Dkt. Biteko ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma Mjini kuendelea kumpa ushirikiano mbunge wao ili aendelee kutimiza majukumu yake ipasavyo sambamba na kuwataka wananchi hao na kutunza amani wakati wa uchaguzi.

“Tunapokwenda kwenye uchaguzi watu wa  Dodoma mmejipanga, Dodoma Jiji imeandikisha watu 628,000, umefanyika utekelezaji mzuri wa Ilani haya yote yamefanyika kwa zaidi ya asilimia 90, na CCM imefanya uhamasishaji mkubwa wakati wa kujiandikisha kwenye daftrari la kupiga kura hivyo hizi ni sababu za kutupa ushindi, wakati wa uchaguzi tuikatae roho ya mgawanyiko na tushikamane kwa ajili ya kujenga chama na na nchi yetu,” ameeleza Dkt. Biteko.

Ameendelea kuwahimiza wana CCM kuwa chama chao ni chama kiongozi na kuwa waendelee kuhamasisha Watanzania kuendeleza misingi ya upendo, mshikamano na umoja sambamba na kuwa na upendo kwa vyama vingine vya siasa.

 Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali imeendelea kuipa kipaumbele Dodoma kama Makao Makuu ya nchi  kwa  kuendeleza na kuanzisha miradi mingi itakayofanana na sifa ya makao makuu ya nchi na kuwa wananchi wa Dodoma waendelee kuwa na mshikamano kwa kuwa Serikali inatambua mahitaji yao na inaendelea kuyafanyia kazi.

 “Tunashuhudia kukamilika kwa ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba ambapo Watanzania wote watapata huduma za Serikali katika eneo moja na hivyo kuwaondolea usumbufu kama ilivyokuwa awali kutokana na mtawanyiko wa Ofisi za Serikali. Tunashukuru ujenzi wa Kiwanja kikubwa cha Ndege cha Msalato ambacho kwa sasa ujenzi wake umefika zaidi ya asilimia 75. Kukamilika kwa kiwanja hiki kutasaidia kurahisisha usafiri kwa wananchi wetu na kuchochea maendeleo ya Dodoma na maeneo ya karibu,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Mwaka 2020 hadi 2024, Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde amewashukuru wananchi wa Jimbo hilo kwa kumchagua na kuendelea kumpa ushirikiano katika kazi zake.

Amesema kuwa Jimbo lake katika kipindi cha miaka minne limepokea zaidi ya shilingi trilioni 1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ametaja baadhi ya miradi inayotekelezwa katika Jimbo lake ambayo ni ujenzi wa barabara ya pete yenye urefu wa km 112.3 inayojengwa Dodoma ili kuondoa msongamano wa magari na ujenzi wa uwanja wa kudumu kwa ajili ya Maonesho ya Wakulima ya Nanenane.

Ameongeza kwa kusema “Mhe. Rais Samia ametoa maelekezo unajengwa uwanja mkubwa wa mpira wa miguu hapa Nzuguni, Dodoma. Kwenye vituo vya afya na zahanati tumepokea fedha nyingi na kazi nyingi zinaendelea sambamba na ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya inayojengwa katika Kata ya Nala,”

Mhe. Mavunde ameendelea kutaja miradi mingine ambayo ni nishati ya umeme na kusema kuwa awali katika Kata ya Chihanga na Mbawala hakukuwa na nguzo za umeme na sasa kuna nguzo za umeme na kuwa yamebakia maeneo machache ili  umeme usambazwe katika jimbo la Dodoma Mjini.

Akizungumzia utekelezaji wa ahadi zake katika Jimbo hilo, amesema kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo amegawa zaidi ya matofali 80,000 na mifuko ya saruji elfu 15 katika kata zote ili kuchochea ujenzi wa zahanati.

“Nimegawa mashine za kutotolesha vifaranga kwa akina mama ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha kiuchumi, katika elimu tumegawa vishikwambi kwa walimu vyenye gharama ya shilingi bilioni 1.7, nimegawa kompyuta 102 katika shule za msingi na sekondari,” amesema Mhe. Mavunde.

Amesisitiza “Nimejenga Shule ya Msingi Chiwondo ili kusaidia wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta shule, watoto waliokuwa wanasoma Shule ya Sekondari Ipala niliwahidi nitajenga shule na sasa shule imejengwa na imekamilika,”

Pia,Mhe. Mavunde amesema kuwa Jimbo lake lilikuwa na changamoto kubwa ya ardhi lakini kupitia kliniki za ardhi zilizofanyika zimesaidia kutatua changamoto hiyo kwa kiasi kikubwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Zainab Katimba amesema kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika Jimbo la Dodoma Mjini hususan katika miundombinu ya barabara.

“Katika miundombinu ya barabara mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya miaka minne tumeona ongezeko la bajeti ya TARURA kutoka shilingi bilioni 5.3 hadi 42.6 kwa mwaka kwa ajili ya kuboresha miundombinu, hii ni dhamira ya dhati ya Rais kuona Dodoma inapata miradi ya kimakakati,” amesema Mhe. Katimba.

Amebainisha “ Sasa TARURA inaweza kuhudumia mtandao wa barabara za lami kutoka urefu wa km 154 hadi  km 249 na barabara za changarawe kutoka km 196.4 hadi km 368.2 hapa Dodoma Mjini, imejenga  makaravati 9 pamoja na kupamba jiji hili kwa taa za barabarani 243.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma Mjini, Charles Mamba amesema kuwa mkutano huo ndio ulimpendekeza Mhe. Anthony Mavunde kufanya kazi za kibunge na kupitia mkutano huo pia ataeleza yale ambayo ametekeleza katika Jimbo hilo.

Ameongeza kuwa Dodoma Mjini wako tayari kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na wamedhamiria kushinda nafasi za uenyekiti kwa asilimia 100.

Awali, Dkt. Biteko amekabidhi  baiskeli 223 kwa makatibu wa matawi wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na spika 45 kwa makatibu kata wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Dodoma Mjini ikiwa ni jitihada za Mbunge wa Jimbo hilo kusaidia viongozi hao kuwafikia wananchi kwa urahisi pamoja na kuwezesha ufanyikaji wa mikutano ya hadhara kwa wananchi.

      

Related Posts