Halotel yazindua promosheni ya ‘Kiwashe na Halopesa’

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kupitia huduma yake ya Halopesa imezindua kampeni inayoitwa “Kiwashe na Halopesa” ambapo zaidi ya washindi 700 wataweza kujishindia pesa taslimu pamoja na zawadi mbalimbali katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Novemba 12, 2024 jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Halopesa, Magesa Wandwi, amesema kuwa katika kuadhimisha msimu wa sikukuu, Halotel kupitia huduma ya Halopesa, imetoa fursa kwa wateja wake kuweza kujishindia fedha taslimu na zawadi mbalimbali.

” Tunafuraha kuzindua promosheni hii ambapo kila siku, wiki na mwenzi, mteja ataweza kujishindia hadi shilingi milioni moja pale mteja anapofanya miamala kupitia Halopesa, hivyo tunawaomba wateja kujiunga na Halopesa na kufanya miamala mingi ili waweze kujiongezea nafasi ya ushindi.”amesema Wandwi.

Ameongeza kuwa promosheni hii ni njia moja wapo ya kutoa Shukrani kwa wateja ambao wamekuwa wakitumia huduma za Halotel kwa ujumla huku Halotel inajivunia kuwa sehemu ya maisha ya wateja wao ambapo watapata huduma iliyo bora zaidi.

Kwa Upande wa Ofisa Masoko wa Halopesa, Aidat Lwiza, amesisitiza kuwa huduma hii ya promosheni inahusisha wateja wanaotumia Halopesa kwa kufanya miamala mbalimbali kila siku na kutumia menu ya 15088# au Halopesa App, na wateja wataweza kujishindia zawadi ya fedha taslim kuanzia 50,000, 300,000, hadi 1,000,000 kila siku, wiki na kila mwezi.

“Promosheni hii ni fursa kwa wateja wetu katika kufurahia msimu wa sikukuu kwa kushiriki katika huduma zetu ambapo wateja watapata nafasi ya kushinda huku tukiwahamasisha waweze kutumia huduma za Halopesa ili waweze kushida zaidi “, amesema Lwiza.

Aidha promosheni hiyo imezinduliwa rasmi leo Novemba 12, 2024 huku ikidumu hadi mwisho wa mwezi Januari 2025 na washindi watatangazwa kila siku, wiki na mwezi kupitia mitandao ya kijamii na njia nyingine za mawasiliano, pia wateja wametakiwa kuendelea kutumia huduma za Halopesa katika msimu huu wa sikukuu ili wafurahie zawadi.

Related Posts