Vyuo vitano vyaingia makubaliano ya kufanya tafiti mbalimbali

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Aga Khan (AKU) Dkt. Sulaiman Shahabuddin akizungumza mara baada ya kuisaniana makubaliano ya ushirikiano wa vyuo vitano ya kukabiliana na na mabadiliko ya tabianchi,jijini Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa William Anangisye akizungumza mara baada ya kuisaniana makubaliano ya ushirikiano wa vyuo vitano ya kukabiliana na na mabadiliko ya tabianchi,jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki katika mkutano wa vyuo vitano ,jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja ya vyuo vitano vilivyoingia katika makubaliano ya ushirikiano ,jijini Dar es Salaam.

*Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Aga Khan Amesema ushirikiano huo unakwenda kutoa majibu

Na Chalila Kibuda Michuzi TV

VYUO vitano vimeingia katika makubaliano katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo ya utafiti na elimu.

Makubaliano ya Vitano yamefanyika Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jijini Dar es Salaam pamoja kufuatia na mkutano wa uwasilishaji mada mbalimbali katika maeneo ya utafiti kwa kila Chuo.

Vyuo ambavyo vimesaini makubalino ya ushirikiano ni Chuo Kikuu Simon Franser (SFU) nchini Canada pamoja na vyuo vinne nchini Tanzania ambavyo ni Chuo Kikuu Aga Khan University (AKU), Taasisi ya ya Sayansi na Teknolojia Afrika Nelson Mandela

(NM-AIST), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Aga Khan (AKU) Dkt. Sulaiman Shahabuddin amesema kuwa ushirikiano m

unakwenda kutoa majawabu katika kukabiliana na Mabadiliko yaTabianchi kwa Wanataaluma na watafiti pamoja na kubadilishana ujuzi wenye utatuzi wa ubunifu

Amesema katika uhiriakiano ni hatua muhimu kwenda mbele katika kuimarisha umoja wa utafiti wa kisayansi pamoja na elimu katika kukabiliana na changamoto zilizopo sasa.

Hata hivyo amesema mashirikiano hayo kwa wadau wamepanga kufadhili semina na mikutano ya mwaka katika suala la mabadiliko ya tabianchi na kuongeza kuwa Mashirikiano hayo yataweka daraja kwa wataalam kujadiliana katika masuala ya utafiti na Teknolojia

Aidha amesema katika ushirikiano huo ni fursa katika kutengeneza miradi ya ushauri yenye kuleta matokeo chanya.

Amesema Mabadiliko ya tabianchi ni changamo ya dunia ambayo inahitaji ushirikiano wa taasisi katika kufanya utafiti wa kitaalam pamoja na elimu.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa William Anangisye amesema makubaliano ya vyao yamekuja katika kuongeza nguvu katika kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya mabadiliko tabianchi.

Amesema kuwa vyuo kufanya utafiti ndio kipaumbele katika kutatua changamoto zinazoizunguka jamii na kuja na suluhusho ya changamoto hizo.

“Ushirikiano huo kwa pamoja kufungua milango katika kujengea na uwezo katka kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo hayana madhara kwetu lakini yanachukua sehemu kubwa ya maisha ya watu”Amesema Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Prof Willam Anangisye

“Mkutano huu ni fursa mhumu kwa vyuo vyote kwa sababu ya kushirikisha washiriki wa Kimataifa na watu wenye uwezo na utaalam kujenga hoja”

Ushirikiano huu unakwenda katika kuwakutanisha wanataaluma, Wansayansi pamoja na Wataalam wa mafunzo katika katika eneo la mabadiliko ya tabianchi na fursa ya ushauari wa elimu kwa wanafunzi pamoja na watafiti.

“Ushirikiano utakwenda mbali kwenye utafiti na ubunifu hivyo taasisi zinatakiwa kufanya kazi pamoja katika kutoa elimu ambayo ni faida kwa wanafunzi na vitivo pamoja na wataalam”amesema Rais wa Utafiti na Bunifu wa Chuo Kikuu Simon Franser (SFU) Dugan O’Neil,

“Kutegemeana na rasilimali na wataalam tutawasaidia katika kuwafundisha kufanya utafiti katika maeneo yaliyochaguliwa”amesema

Related Posts