SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine imesema mikakati iliyowekwa katika kukabiliana na migongano baina ya binadamu na wanyamapori imekuwa na mafanikio chanya.
Hayo yameelezwa na Ofisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Antonia Anthony wakati wa mjadala kuhusu migongano baina ya binadamu na wanyamapori uliondaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ).
Anthony amesema kabla ya kuja na mikakati walibaini visababishi vya migongano hiyo ambavyo vilikuwa ni uingizaji mifugo kwenye hifadhi, kukosekana, kutokuzingatiwa au kuisha muda wa mipango ya matumizi ya ardhi ngazi ya mikoa,wilaya na vijiji.
Pia sababu nyingin ni mabadiliko ya tabianchi (Ukame na mafuriko) ; na ongezeko la mimea vamizi katika maeneo yaliyohifadhiwa hali ambayo huzuia uoto wa mimea ya asili ambayo ni malisho ya wanyamapori.
Amesema athari za visababishi hivyo ni uharibifu wa mazao na miundombuni; mifugo na binadamu kujeruhiwa/ kuuawa.Pia serikali ilianisha mikakati 15 ya kudhibiti migongano hiyo ambapo mafanikio yameonekana kwa asilimia kubwa.
“Tuliandaa mkakati wa Taifa wa Kusimamia Utatuzi wa Migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori (2020-2024); Mkakati wa Kusimamia na Kuhifadhi Tembo nchini (2023-2033); naü Mkakati wa Kuongoa Shoroba za Wanyamapori nchini (2022-2026),” amesema.
Ameongeza mkakati wa kuongoa shoroba za wanyamapori umebainisha shoroba 61 ambapo shoroba 20 zimepewa kipaumbele kuongolewa na nane zipo katika hatua mbalimbali za uongoaji ukiwemo Selous-Niassa (Ruvuma) na Selous-Nyerere-Udzungwa (Ruvuma na Morogoro).
Anthony amesema shoroba ya (Nyerere-Selous Udzungwa) umekamilika ambapo hatua inayofuata ni kupata Tangazo la Serikali (GN).Shoroba zingine ni Ruaha-Rungwa – Udzungwa, Ruaha Rungwa – Katavi, Ziwa Manyara- Tarangire, Ziwa Manyara – Ngorongoro- Serengeti, Ngorongoro- Ziwa Manyara, Selous – Niassa Mabango, Katavi – Mahale, Nyerere – Selous – Udzungwa.
“Hatua iliyofikiwa Wizara kwa kushirikiana na wadau imeandaa rasimu ya mwongozo wa kuongoa shoroba utakaotumika pia katika zoezi la uwekaji wa mabango kwenye shoroba 20 ukiwemo Selous Niassa,” alisema.
Amesema Wizara imeshirikiana na wadau (STEP, USAID, SADC – TFCA, WCS), WWF, KfW kuongoa shoroba hizo ambapo (Nyerere-Selous Udzungwa) umekamilika na wanyamapori
wameonekana kuanza kupita.
Ametaja mkakati mwingine ni doria maalum za udhibiti wa mifugo hifadhini ambapo mwaka 2023/24 jumla ya mifugo 2,152 ilikamatwa kwenye maeneo ya hifadhi katika ukanda wa Ruvuma.
Pia kuwezesha mipango ya matumizi ya ardhi ambapo mwaka 2024/2025 wanatarajia kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 74 katika Wilaya za Bunda (28), Kisarawe (6), Ulanga (5), Liwale (6), Tunduru (8), Tanganyika (11) na Uvinza (10)
“Pia tumefanikiwa katika mkakati wa uchimbaji wa mabwawa 30 katika hifadhi za taifa za Serengeti, Nyerere, Saadani, Mikumi, Tarangire na Mkomazi na mapori ya akiba ya Selous Liwale, Rungwa, Kizigo, Muhesi, Maswa, Msanjesi, Ruaha na Katavi,” alisema.
Mikakati mwingine ni kuboresha maeneo ya malisho ya wanyamapori ambapo mwaka 2023/24 mimea vamizi iliondolewa katika eneo lenye ukubwa wa hekta 3,776.57 katika hifadhi za Taifa mbalimbali
Amesema pia wamefanya doria za udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu ambapo katika kipindi cha kuanzia 2023/2024 jumla ya matukio 1,806 yalidhibitiwa katika Ukanda wa Ruvuma.
Amesisitiza wamejenga vituo vya askari wanyamapori 154, wametoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi 177,851 katika kipindi cha mwaka 2023/2024 na katika kipindi cha 2021/2022 hadi
2023/2024, mafunzo yalitolewa kwa wakufunzi 1,650 katika wilaya 29 zenye changamoto zaidi na wakufunzi 197 walitoka Ukanda wa Ruvuma katika Wilaya za Tunduru, Namtumbo, Liwale, Nachingwea, Ruangwa, Lindi (Mtama na Mchinga).
Ofisa huyo amesema mpango wa mwaka 2024/2025 ni kutoa mafunzo wa Askari Wanyapori wa Vijiji (VGS) 200 kutoka Wilaya 44 na wakufunzi 320 katika wilaya 16 zenye changamoto.
Anthony amesema matumizi ya teknolojia (GPS Satellite Collars & Drones) ni mkakati mwingine ambao umeleta ufanisi.
Kwa upande Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Wanyamapori, Dk Fortunata Msofe alisema kupita mradi huo wameweza kutoa mafunzo kwa waalimu wa waalimu (59) na wakulima 1550.
Pia wamefundisha mbinu za kuzuia uharibifu mashambani ikiwemo ufungaji uzio wa harufu mbaya katika eneo la ukubwa wa kilomita 23 na wakulima 280 waliolima ekari 1300 katika vijiji 24 wamenufaika.
“Tumeimarisha programu ya wilaya ya kutatua migongano, mafunzo ya kilimo bora kwa kushirikiana na SWISS AID, mpango wa kuwawezesha VGS kiuchumi (VETA) na wa vikundi vya kijamii