“HABARI YA UPENDO, USHIRIKIANO, UMOJA NA MSHIKAMANO VIMETOWEKA KWA SIKU ZA HIVI KARIBUNI” – CP TENGA

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

IMEELEZWA Kuwa swala la Upendo, amani, mshikamano na ushirikiano ni tunu ambayo inaonekana kwa siku za hivi karibuni inapotea.

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Nchini (CP) Nicodemus Tenga alipomuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Magereza katika mkutano wa maafisa na askari waliofanya mafunzo ya awali pamoja ya uaskari Magereza (Depo) namba 12 ya mwaka 1994.

Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Msalato jijini Dodoma

CP. Tenga amehimiza upendo, ushirikiano, kusaidiana, na kufanya kazi kwa bidii ili kuliletea Jeshi la Magereza sifa nzuri.

“tumekutana hapa na wenzetu kutoka idara mbalimbali nje ya Jeshi la Magereza pamoja na wale waliotoka mikoa mbalimbali, lengo kubwa ni kushuhudia jambo hili kubwa ambalo limefanywa na Depo namba 12 hawa wenzetu wanatuimiza tupendane, tushirikiane, tuthaminiane na tujaliane katika shida na raha. Hii itatuweze kufanya kazi kwa weledi na kuliletea Jeshi letu sifa nzuri,” alieleza Kamishna Tenga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Kozi ya Kijeshi namba 12 ya mwaka 1994, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Joyce Mkufya,amesema jambo hilo waliofanya kwa kukutana pamoja na kutoa msaada kama huo wao wameanzisha jambo hilo na ameshauri DEPO nyingine waone uwezekano wa kufanya kama wao kwa sababu ni jambo la kizalendo

Akitoa neno la shukrani mbele ya uongozi wa Jeshi la Magereza kwa niaba ya wanajumuiya wa Depo namba 12, Mheshimiwa Saraji Iboru, ambaye ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Kesi na Utaratibu wa Upelelezi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, alipongeza uongozi wa Jeshi la Magereza kwa maendeleo makubwa ambayo yamefikiwa pia wanajumuiya wa Depo namba 12 kwa msaada walioutoa kwa Jeshi la Magereza, akisisitiza kuwa msaada huo utasaidia jeshi kutekeleza mipango na mikakati yake, ikiwemo ujenzi wa Hospitali na Maabara ya kisasa yenye hadhi ya Wilaya, ambayo itasaidia kutoa huduma bora za afya kwa makundi mbalimbali katika jamii.alieleza Mhe. Saraji Iboru.




Related Posts