Polisi kuchunguza tukio la kupigwa risasi kada wa CCM Iringa

 

JESHI la Polisi Mkoani Iringa kupitia kwa kamanda wa mkoa huo Allan Bukumbi, limesema linachunguza tukio la kupigwa Risasi kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Kilolo, mkoani humo Christina Kibiki, mkazi wa kitongozi cha Banawanu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Tukio hilo lilitokea tarehe 12 Novemba 2024, ambapo kwa mujibu wa uchunguzi wa awali uliofanywa na jeshi hilo umeeleza kuwa, kada huyo alivamiwa na watu watatu ambao hawakufahamika, na kumshambulia kada huyo na familia yake na kisha kutoweka.

Taarifa ya polisi inaeleza kuwa, licha ya watu hao kumshambulia Christina na kupelekea kupoteza Maisha, wahalifu hao hawakufanikiwa kuondoka na kitu au mali yeyote kutoka kwenye nyumba ya kada huyo.

Wakati jeshi hilo likiendelea na uchunguzi, Chama cha Mpinduzi kupitia katibu wake wa NEC, Itikadi na uenezi Amos Makalla, kimeonesha kusikitishwa na tukio hilo sambamba na kutoa pole kwa ndugu, familia na wanachama wao.

Aidha jeshi la polisi limeendelea kusisitiza kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu wahalifu, azifikishe kwenye mamlaka husika ili ziweze kufanyiwa kazi.

About The Author

Related Posts