Spika wa IPU Azungumza katika mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Nairobi Jijini Nairobi nchini Kenya

Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Tulia alikabidhi nafasi ya Mwenyekiti kwa Spika wa Bunge la Kenya Moses Wetang’ula.

Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akipeana mkono na Spika wa Bunge la Kenya Mheshimiwa Moses Wetang’ula mara baada ya kumkabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Maspika wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Tulia ameshika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Maspika wa EAC uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maspika wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati walipohudhuria Mkutano wa Maspika wa nchi hizo uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson wa kwanza kulia akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Uganda Mheshimiwa Anita Among na Spika wa Bunge la Mpito la Sudan ya Kusini Mheshimiwa Jemma Kumba wakati walipohudhuria Mkutano wa Maspika wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.

Related Posts