Mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki Wafikia Asilimia 47.1, Utekelezaji Watarajiwa Kukamilika 2026

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema kuwa hadi sasa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (Hoima, Uganda-Tanga, Tanzania) umefikia asilimia 47.1 na unatarajia kukamilika Julai, 2026.

Mradi huo ni Moja ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa kwa Ushirikiano kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (15%), serikali ya Jamhuri ya Uganda (15%), Kampuni ya Total Energy (62%) toka Ufaransa na Kampuni ya CNOOC (8%) kutoka Jamhuri ya watu wa China.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mradi wa Bomba kutoka TPDC, Asiadi Mrutu amesema mradi huo unafuatia ugunduzi wa mafuta nchini Uganda yenye jumla ya ujazo wa mapipa bilioni 6.5.

Amesema utwaaji wa ardhi umezingatia matakwa ya Sheria ya Ardhi ya Tanzania ma taratibu za kimataifa ili kuhakikisha kunakuwa na usawa, haki na ushirikishwaji wa Wananchi waliopo kwenye maeneo ya mradi.

“Upande wa Tanzania ardhi ya mradi wa bomba ina eneo lenye urefu wa kilomita 1,147 na upana wa mita 30 ambapo kwa upande wa Tanzania kilometa hizo zote jumla ya wananchi 9,927 wameguswa na mradi sawa na wastani wa watu 9 Kila kilomita 1.

“Kati ya wananchi 9,927 ni wananchi 344 pekee ndio wamepoteza nyumba za makazi sawa na asilimia 3.4. Aidha kati ya wananchi 344 wananchi 50 walichagua kupewa Fedha taslimu na wananchi 294 walichagua kujengewa nyumba za makazi mbadala,” amesema.

Amefafanua kuwa, mpaka Oktoba 31, mwaka huu jumla ya Nyumba zote 340 zimejengwa na kukabidhiwa kwa wananchi 294 sawa na asilimia 100 huku serikali kushirikiana na mradi imefanikiwa kuainisha mikataba ya malipo ya fidia kwa wananchi 9858 ambapo wamekwishalipwa jumla ya mikataba Sh. Bilioni 35.1 sawa na asilimia 99.3.

“Wananchi 69 waliobaki wanaendelea kutatua changamoto mbalimbali na kukamilisha taratibu ili waweze kusaini mikataba na kulipwa fidia,” amesema.

Ameeleza tangu kuanza kwa mradi huo Februari 2022 umeweza kununua Huduma na bidhaa za ndani ya nchi zenue thamani ya jumla ya Dolla za Kimarekani 304.95 sawa na takribani shilingi Bilioni 821.1 .

Hata hivyo amesema mpaka Septemba 30 mwaka huu mradi umetoka fursa za ajira Kwa Watanzania 8694 kupitia wakandarasi kwenye maeneo mbalimbali .

“Inakadiriwa kipindi hiki cha ujenzi wa Bomba lenyewe jumla ya Watanzania 7030 watapata fursa za ajira kwenye maeneo mbalimbali ya ujenzi ambapo mpaka sasa Watanzania 6430 wanafanya kazi kwenye mradi ambapo wengi wao wao kwenye maeneo ya ujenzi na baadhi kwenye ofisi za wakandarasi zilizopo Dar es Salaam .

Ameongeza kuwa mara ujenzi utakapokamilika Kampuni ya EACOP inatarajia kuwa na jumla ya wafanyakazi 148 ambapo 114 watatoka Tanzania na 34 watatokea Uganda.

Related Posts