Rais Mwinyi awaapisha kadhi na katibu mtendaji wa tume ya utangazaji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Mhe.Iddi Said Khamis kuwa Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa.

Pia Ndugu Hiji Dadi Shajak kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji.

Hafla hiyo ya uapisho uliofanyika Ikulu Zanzibar tarehe 14 Novemba 2024 umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdullla , Mawaziri, viongozi wa Dini na Vyama vya siasa.

   

Related Posts